WASICHANA 170 WANUSURIKA KUKEKETWA HANDENI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Handeni. Jumla ya wasichana  170 wenye umri kuanzia miaka mitano mpaka 14 kutoka jamii ya wafugaji kijiji cha Kang’ata wilaya ya Handeni mkoani Tanga wamefanyiwa sherehe ya kuvushwa rika bila kukeketwa baada ya wazazi wao kupewa elimu za athali ya kitendo hicho.

Akizungumza kwenye sherehe hizo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Noel Abel kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo, Godwin Gondwe amewapongeza viongozi wa kimila wa jamii ya kimasi kwa kukubali elimu waliopewa na shirika la Amref kwa kuacha ukeketaji.

Amesema ukeketaji ni moja ya mila hatarishi Tanzania ambayo inaathiri afya ya uzazi ya mwanamke ikiwemo kuambukizwa virusi vya ukimwi na madhara wakati wa kujifungua.

Meneja mradi wa Kijana wa Leo kutoka Amref  wilaya ya Handeni, Dk Aisha Byanaku amesema lengo lilikuwa ni kuwafikia wasichana 160 katika mwaka wa kwanza wa mradi  na wamevuka kwa kupata 170 ambapo kwao inaonyesha mafanikio.
Post a Comment
Powered by Blogger.