SUMU YA PENZI SEHEMU YA THELASINI NA SABA(37)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Nikarudi zangu nyumbani nikiwa namnyonyesha mwanangu, ilipofika jioni mume wangu alitaka kutusapraizi kwa kutupeleka familia nzima kwenye baa moja ili kunywa pombe, lakini alinisisitiza na mimi kuwaleta rafiki zangu aliowaona ile asubuhi.
Basi nikawataarifu marafiki zangu Catherine na Getrude, mida ilipofika wakaja lakini nilisahau kabisa kuwaambia wasimwambie kimbelembele Fatuma, maana alikuja tena kwa kuwahi kuliko wote akiwa amechana minywele yake na kuifunga na kilemba.
Baadaye walikuja akina Cathe wakiwa wamependeza mno mawigi ya bei mbaya, magauni yao wakionekana kama vile wamevunja kabati. Na mimi nikaamua kuingia zangu ndani, nikajikwatua ile mbaya na mipodozi yangu ya Kimarekani nikatoka nikiwa poa sana hadi kila mtu akanitamani.
Mume wangu alipoingia ndani alinisifia tu mara moja kisha akawasalimia mashoga zangu lakini aligeuka na kumtazama Fatuma kwa muda tena akatabasamu kabisa. Hilo nililiona likanikera mno.
Basi pamoja tukatembea tu  nakuelekea kwenye baa ya Kivulini na kupozi zetu tukazungusha meza kama nane hivi nakufanya mzunguko mkubwa, mama alikuwepo, dada zangu, wajomba, mashangazi, rafiki zangu, baba na majirani kibao, basi zikaanza raundi. Wasio kunywa bia wakaishia kwenye soda tu.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA


ITAENDELEA JUMATANO
Post a Comment
Powered by Blogger.