SUMU YA PENZI SEHEMU YA THELASINI NA NANE(38)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Basi kama kawaida mchana nikaenda zangu kupiga stori kwa rafiki zangu, nikawakuta wamejaa tele tena na Fatuma naye alikuwepo lakini siku hiyo alikuwa tofauti sana, alionekana mwenye furaha na amejaa maneno mdomoni kweli.
Nililigundua hilo nikapanga kumshusha kwa sababu mkuu wa kundi nilikuwa nimeshafika  tena kila kona nikipewa sifa kuwa nimeolewa na Mmarekani, yaani nilionekana kama vile shujaa kwenye jamii nzima ya wanawake pale mtaani.
“jamani mamboz!” niliwasalimia tukakaa na kuanza kupiga stori za jana kuhusu kule baa.
“mh mimi si unajua nalea, yaani pombe nilikunywa muda kweli  basi jana ile kuonja tu zikanibeba,” nilisema.
“mimi mwenzenu aku! Nilikunywa hadi mwisho, nadhani hata kreti nililimaliza,” aliropoka Fatuma akichekacheka. Na kweli kwa kile kiumbo chake chembamba acha amalize kreti, hajaolewa, hajazaa anapresha gani! Niliwaza akilini lakini nikataka kumshushua kwa maneno pia ili aache kidomodomo.
“unajua Fatuma saa nyingine nakuonaga kama una matatizo? hivi umeshawahi kwenda kwa mganga angalau akujalie upate bwana, utakaa na bibi hadi lini?” nilipiga dongo makusudi.
“Mungu ndiye anayepanga, kama amenitaka nizeeke peke yangu sawa,  kwani kuolewa kitu gani bwana!” alisema kwa kujiamini.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA ALHAMISI 

Post a Comment
Powered by Blogger.