MSANII DARASSA AWEKA REKODI NYINGINE MOSHI

Huenda huu ukawa ni wakati mzuri kuliko katika maisha yote ya muziki ya msanii Darassa CMG, kutokana na makubwa ambayo anayafanya kwasasa baada tu ya ngoma yake ya Muziki kufanya poa kinoma noma mtaani.

Huwezi kuwataja wasanii ambao wanakinukisha kinoma noma kwa suala zima la shows kwasasa hapa Bongo ukaacha kumtaja Darassa. Ukiachana na mashavu ambayo alikuwa akiyapata kwenye majukwaa ya Fiesta, Darassa ni msanii ambaye ameendelea kukonga nyoyo za mashabiki kwenye kila show anayofanya.

Exclusive ambayo nataka kukupa muda huu kumuhusu mkali huyo ni show ambayo ameifanya usiku wa Christmas pande za Moshi, show ambayo taarifa zinasema kuwa ukimbi ulijaa kiasi kwamba kutoruhusiwa mtu kuingia tena ndani ya ukumbi huo (Sold Out). Ni rekodi katika historia ya muziki wa Hiphop kwa hapa kwetu Bongo.

Nakupa nafasi ya kutazama angalau kwa kiduchu jinsi alivyofanya mkali huyo kwenye show hiyo ya Moshi
Post a Comment
Powered by Blogger.