Miili 10 ya waathiriwa wa ndege Urusi yapatikana


Urusi imetangaza kupokea miili 10 ya waathiriwa wa ile ajali ya ndege iliyotokea katika bahari ya Black Sea hapo siku ya Jumapili.

Maiti hizo zimesafirishwa hadi mji mkuu- Moscow, Abiria wote 92 waliangamia katika ajali hiyo baada ya kupaa angani muda mfupi kutoka Sochi.

Waziri wa usafiri nchini humo Maxim Sokolov, anasema hitilafu za kimitambo ama makosa ya rubani huenda ndio iliyosababisha ajali hiyo.

Shughuli za utafutaji zinaendelea, Wanasayansi wa Urusi wanakusanya chembechembe za DNA kutoka kwa jamaa za waathiriwa, ili kuweza kuzitambua maiti hizo.
Post a Comment
Powered by Blogger.