HIKI NDICHO DOGO JANJA ANACHOJUTIA ZAIDI MAISHANI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Dogo Janja ambaye wiki kadhaa zilizopita amempoteza baba yake mzazi, alikiambia kipindi cha 'Ngaz Kwa Ngaz' kinachoruka kupitia EATV kuwa katika maisha yake anajutia kukosa shule na anasema katika kipindi ambacho alikuwa shule hakuwahi kupata experince ya mitihani ya kujipama jambo ambalo lilichangia yeye kufeli shule na kushindwa kuendelea na masomo.

"Unajua kila siku maneno yapo na yanasemwa lakini mimi katika maisha yangu mpaka leo kitu ambacho nakijutia sana ni kukosa shule, nakumbuka ilivyokuwa ni kipindi ambacho nilikuwa nimetoka Tip Top Connection kwa hiyo nilirudi Arusha ndiyo kipindi nilikuwa form two na ndiyo kipindi cha mitihani ya mock kilikuwa kimekaribia, kwa hiyo wenzangu walifanya mimi sikufanya hivyo sikupata experince ya mtihani iko vipi, inakujaje kujaje harafu nilikaa sana Arusha na niliporudi tu mjini wiki tatu tu mtihani wa taifa huu hapa kwa hiyo nilifeli, hata kufeli kwangu hakukuwa kwa maksi kubwa japo kuwa nilipitwa na vitu vingi" alisema Dogo Janja. 
Post a Comment
Powered by Blogger.