CAF yatangaza majina 3 ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika

Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) limetangaza majina ya wachezaji watatu ambao watawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka huu.

Wachezaji waliotajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon (Borussia Dortmund), Riyad Mahrez wa Algeria (Leicester City) na Sadio Mané wa Senegal (Liverpool).
Wachezaji wengine waliotajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ligi za ndani kwa ligi za ndani ni golikipa wa Uganda Dennis Onyango na Khama Billiat wa Zimbabwe wote wanachezea klabu ya Mamelodi Sundowns na Rainford Kalaba kutoka Zambia na klabu ya TP Mazembe.
Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Januari 5, mwakani jijini Abuja, Nigeria.
Post a Comment
Powered by Blogger.