UPDATES: MBUNGE WA JIMBO LA DIMANI(CCM), NDG. HAFIDH ALI TAHIR AFARIKI DUNIAMhe. Hafidh Ali Tahir amefariki dunia saa 9 alfajiri ya kuamkia leo katika Hospitali ya General hapa Dodoma.

Marehemu alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.

Marehemu pia alikuwa mwamuzi wa FIFA na mwana-Yanga kindakindaki na ni jana tu amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Tawi la wabunge wanaYanga mjini Dodoma chini ya Uenyekiti wa Venance Mwamoto.

Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitakuijia hivi punde.
Post a Comment
Powered by Blogger.