SUMU YA PENZI SEHEMU YA KUMI (10)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Baada ya kumpokea na kumpikia na kumpakulia kama kawaida nilitangulia kulala na kumuacha mume akiendelea na makazi yake ya makompyuta. Mimi nikalala zangu kimya huku nikiwaza na kuwazua kichwani nikiwa na maswali kibao.
La kwanza lilikuwa ni kumfahamu yule mwanaume aliyekuja pale chumbani ni nani?  “Atakuwa Dr Ben nini?” nilijiuliza kwakuwa nilijua tu kama siku moja na mimi nitakubuhu kufikia kufanya aliyokuwa akiyafanya Blandina basi sitakuwa na chaguo zaidi ya kufanya na mwalimu ambaye ni Dr.Ben.
Nikatamani hata yule mwanaume aliyekuja mle chumbani awe ndiye yeye. Nikaanza kumvutia picha ya jinsi alivyokuwa nikajikuta nikimfananisha kila kitu na Dr.Ben.
Lakini siku hiyo nililala nikiwa na mtazamo mpya kichwani mwangu kuhusu suala zima la mapenzi. Tayari nilikuwa nimeishaanza kuamini kuwa raha ya mapenzi ni kumpata mpenzi anayejua mapenzi, nikahisi nimekosea hata kuolewa mapema nikajisema bora ningekutana na Dr.Ben kwanza.
Niliendelea na kazi zangu nyumbani nikila na kunawili na kwa wakati huo hata vichocheo vyangu vya mwili vilikuwa vimeamka na kunifanya kila baada ya siku chache nijisikie msisimko ambao mume wangu hakuwa mkunaji.
Hauwezi amini nikawa kila nikiwaza namuwaza yule mwanaume aliyekuja na ile maski usoni. Ilifikia wakati kila nikiona mwanaume wa hivi hata kwenye televisheni nikawa namkumbuka yule mwanaume.
Siku zikakatika hatimaye wiki, nikaanza kufikiria kumpigia Blandina ili anipe ratiba ya darasa. Nilipompigia akaonekana kunichangamkia lakini nilipomwambia kuhusu darasa akaniambia kuwa Frank anaumwa mafua hivyo yeye hatakuwa kwenye mudi lakini akama nikitaka kama kufika kwa ajili ya mafunzo ya kawaida basi nakaribishwa kwa kuwa darasa ni siku hiyo.
Basi mie nikajifanya naenda kwa mawili, la kwanza kumpa pole shemeji Frank la pili ni kujifunza 
Nilifika na kuingia ndani nikawakuta wakiwa wamekaa sebuleni wote, shemeji yangu Frank akionekana kweli ana  mafua sana maana hata sauti yake ilikuwa haitoki vizuri.
Kama kawaida baada ya kufika tuliinuka na kuingia kwenye kile chumba chetu cha makamuzi, na mimi siku hiyo nikiwa mwenyeji haswa.
Lakini macho yangu yakawa yakimuangalia Dr.Ben muda wote huku nikimtamani hasa kwa ile staili aliyokuja nayo ya kujificha uso wake. Lakini mwenyewe alikuwa haoneshi dalili zozote za kumtazama Mary hasa kutokana na kitendo chake cha jana yake cha kumkimbia wakiwa kule korokoroni.
Mary akaanza kuwa na wasiwasi kuwa pengine hakuwa Dr.Ben ambaye aliingia mle chumbani. Akamtazama mume wa shoga yake lakini akaona hakuwa yeye na uwezekano ulikuwa kwa Dr. Ben pekee.
“Leo tutajifunza kuhusu ‘sexual fantancies’ kwa kiswahili sina maana kamili lakini ni kama matamanio ya kuona kitu kwa mfano wa taswira uliyoiumba wewe mwenyewe, hiyo ndiyo fantancy. Linapokuja suala la sexual fantancies maana yake hizo taswira umbishi zinahusu mapenzi tu. Na si kitu kingine.
  

ITAENDELEA ALHAMISI
Post a Comment
Powered by Blogger.