'SCORPION' AONGEZEWA SHTAKA JINGINE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) amemuongezea shtaka lingine mshtakiwa Salum Njwete maarufu kama Scorpion na sasa atakuwa na mashtaka mawili ya unyang'anyi wa kutumia silaha na shtaka la kujeruhi.
Scorpion aliongezewa shtaka hilo jana na Wakili wa Serikali Nassoro Katuga, kabla ya kumsomea Maelezo ya Awali (PH).
Baada ya kusomewa maelezo ya awali, Scorpion alikubali hoja mbili na sita kuzikana.
Kutokana na maelezo hayo, hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Flora Haule aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 14, mwaka huu kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.
Mshtakiwa amerudishwa rumande kutokana na moja ya shtaka linalomkabili kutokuwa na dhamana.
Post a Comment
Powered by Blogger.