NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA TISINI NA SITA(96)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“Ni rahisi tu, nilimuwekea sumu kwa sababu alifahamu siri zetu, unaweza kushangaa nilivyoweza kuwa na mtandao mkubwa jeshini kiasi kwamba hata Generali mwenyewe hakujua kama alikuwa ameandaliwa mtego kabambe wa kumpoteza uhai wake,” alijibu Luteni Generali.
“siri gani kubwa hadi mkaamua kumuua Generali!” aliuliza tena Tinonko, Luteni Generali Mwakabuku akiwa hana wasiwasi alimtazama Tinonko kwa muda.
“sijui kama kufahamu kutakusaidia chochote, niwe mkweli Tinonko kwa kipindi kifupi nimetokea kukupenda sana hasa kwa kale kaujanja kenu ka kumficha General, lakini muda ujao nadhani Mungu atakupenda zaidi. “Sasa anza kuniambia kuhusu hazina za Kongo ambazo wewe unazo. Sina muda mwingi. Kama hautasema chochote, nitahesabu hadi tatu na nitaamuamuru mtu akuue hapahapa, mpo wengi sitapungukiwa na taarifa,” alisema Luteni Generali Hashimu akampa ishara Meja Generali, Seba na wenzake kuwa anachokiongea hana masihara nacho hata kidogo, hivyo wakaandaa bastola zao na kumuelekezea Tinonko.
“Moja! Mbili! ..” alianza kuhesabu Luteni Generali Hashim, lakini akakatishwa na mlio wa simu ya Meja Generali Charles aliyeomba radhi na kupokea. 
akaongea kwa muda na kurudi kwa Luteni Generali.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.


ITAENDELEA JUMAPILI
Post a Comment
Powered by Blogger.