NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA TISINI NA SABA(97)


NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA TISINI NA SABA(97)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“Haya Luteni Generali Hashim tukio zima linarushwa laivu kupitia televisheni ya taifa, haina haja ya kuendelea na chochote dhamiira yako imeshaonekana,” aliongea Generali Mwakabuku akijidhihirisha kwa mara ya kwanza mbele za wote kuwa hajafa na ni mzima kiafya.
Waandishi wa habari wakaanza kupiga picha huku wengine wakitaka hadi kumhoji Generali Hashim na Meja Generali Charles walioganda kama mazombi waliokosa nyama za kula. Wakati huo timu ya watu wa huduma ya kwanza walikuwa wakihangaika kumhudumia Tinonko wakijitahidi kuzuia damu iliyokuwa ikimtoka kwa wingi kifuani pake.
“Mungu wangu! tumekwisha!” alinong’ona Luteni Generali Hashimu akimwambia Meja Generali Charles.
“Niliwashtukia mapema na ndiyo maana na mimi nimewaandalia sapraiz yao, sitakubali kukamatwa kirahisirahisi, nitakufa na wote humu,” alisema Meja Generali Charles, Luteni Generali akashtushwa na kauli hiyo akamtazama mwenzake na kugundua alikuwa na bomu aina ya guruneti, ‘hand grenade’ alilolishikilia vyema mkononi mwake.
“Jamani bomuuu! “ alipiga makelele Luteni Generali Hashimu kwa hofu kubwa huku akikimbia lakini huko nje akazuiwa na kuwekwa chini ya ulinzi. kelele hizo ziliwafanya watu waliokuwemo humo kuanza kukimbilia kila mmoja kwake, Meja Charles akiwa mwepesi mno akamuwahi rais Mrisho na kumshikilia nganganga.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.

ITAENDELEA JUMATATU
Post a Comment
Powered by Blogger.