NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA TISINI NA TANO(95)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“Ulikuwa unataka kumwambia nini rais?” aliuliza Luteni Generali Hashim mara tu baada ya kufika ofisini kwao jeshini makao makuu.
“Aah nilitaka tu kumwambia, kuhusu akina Tinonko,” alidanganya Meja Generali Hashimu maana alishaanza kuona uso wa Luteni Generali ukianza kubadilika.
“Kuhusu akina Tinonko? Kipi hasa ulichotaka kumwambia ambacho hukuona umuhimu wa kunishirikisha mimi kabla,” aliwaka Luteni Generali na laiti kama angejua lengo la Meja Generali lilikuwa kumsaliti mbele ya rais nadhani angemnyongelea hapohapo.
“Nilitaka kumwambia kuhusu siri za mali za akina Tinonko, najua hilo lingemfanya rais aje upande wetu,” alitunga uongo Meja Generali.
“sasa mbona haukuniambia chochote? kuna siri gani hapo sasa. Sikia iwe rais anakuja kwetu au haji kwetu lakini lazima atafanya kama tunavyotaka! Tena hana kauli mbele yangu, wewe subiri uone kesho.”
“Mkuu hapo lazima akupandishe tu cheo, kwa yale uliyomwambia leo nilimuona rais akitetemeka,” alijikomba Meja Generali akijifanya kumsifia Luteni Generali Hashim ambaye naye kwa kulewa sifa akasema; “Hahaaa mimi siyo mtu wa mchezomchezo.” Wakati wakisema hivyo mara simu iliingia usiku huo kutoka kwa Seba akitoa taarifa kwamba Tinonko ameonekana peke yake akitokea hapo jeshini kuelekea nyumbani kwake tena akionekana kuchelewa mno kutoka siku hiyo.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.


ITAENDELEA JUMAMOSI
Post a Comment
Powered by Blogger.