NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA TISINI NA NNE(94)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Siku tatu zikapita huku kila mmoja akipanga mikakati yake, Luteni Generali Hashim akiwa anaamini kuwa yupo pamoja na Meja Generali Charles, akapanga safari ya kukutana na rais ana kwa ana.
Hakuona haja ya kumwambia Meja Generali Charles, badala yake alimpitia tu ofisini kwake na kwenda naye moja kwa moja ikulu, Meja Generali Charles alianza kupata wasiwasi kwa sababu kama angefahamu kuwa walikuwa wakielekea Ikulu sidhani kama angekubali, hiyo inatokana na ukweli kwamba, alikubaliana na rais kukutana naye siku mbili nyuma ila alighairi bila kumwambia, hivyo aliombea ikiwa rais atakuwepo ikulu basi asikumbuke.
Gari iliingia bustani za Ikulu sasa ikawa inaelekea kwenye parking, na wao wakashuka na kuingia moja kwa moja ndani. Rais Mrisho aliyekuwa akipitia mafaili kadhaa kwenye ofisi yake alishtuka kutokana na ujio huo usio na taarifa, lakini aliamua kuongea nao chochote.
“samahani kwa kuja bila taarifa mkuu,” alianza kuomba radhi Luteni Generali Hashimu.
“Enhe nini kilichowaleta leo,” alisema rais huku akijifanya yupo bize mno kiasi cha kutowaangalia usoni.
“mkuu nadhani unafahamu kuwa cheo cha Generali hakina mtu hadi sasa, na mimi ndiye pekee ambaye kiprotokali napaswa kupewa cheo hicho, hata wewe mwenyewe uliniambia hilo,” alianza kutikisa kiberiti Luteni Generali wakati huo Meja Generali Charles alitulia kimya.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.


ITAENDELEA IJUMAA
Post a Comment
Powered by Blogger.