NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA TISINI NA TISA(99)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


"Hivyo ndivyo ambavyo viongozi tunaowaamini kwenye serikali wanapotumia kila njia kutushusha chini na wao kuwa juu kila siku.
“mimi ni mwanajeshi tu ambaye nimejua siri hiyo na nimetaka Watanzania na watu wote duniani tuijue na tunufaike nayo. Wasalaam mimi ni Meja Generali Charles Mtanzania mzalendo," alisema kisha mbele ya kamera akaliweka bomu lake chini na kuwafungulia akina Tinonko na rais mwenyewe kisha yeye akanyanyua mikono juu ishara ya kujisalimisha akijua fika kuwa amejisafisha amesafishika.
Kilichofuatia hapo ni Komando Deo kumvamia Meja Generali Charles na kumshushia kipigo kikali ambacho kilionekana laivu kwenye televisheni, lakini tayari walikuwa wamechelewa mno, akili ya Watanzania na dunia nzima ikawaona wao ni maadui na walikuwa wakimpiga mtu aliyetetea haki za wengi.
Huwezi amini hata askari walipoingia ndani walikuwa na oda kutoka kwa IGP Mapunda kumkamata Rais, akina Komando Deo ambapo Tinonko alionekana kupona haraka kuliko kawaida yaani ndani ya saa chache alikuwa mzima huku zile damu zikiwa kama sio zake.
Wakati hao wakikamatwa, Meja Generali Charles alikuwa ni shujaa aliyepokelewa kwa heshima akistahili kuvikwa vyeo vya kila aina.UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.


ITAENDELEA  JUMATANO
Post a Comment
Powered by Blogger.