NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA TISINI NA TATU(93)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kwa maneno hayo Meja Generali Charles akajikuta yupo njia panda, hakujua kama Luteni Generali Charles alikuwa na siri nzito kiasi kile, unajua Askofu John Mshagama alikuwa ni kiongozi wa kanisa fulani hivi lenye waumini wengi enzi hizo.
Lakini alianza kujiingiza zaidi kwenye siasa kuliko dini kiasi cha kanisa zima kuwa ni taasisi tu kwa sababu lilibakia jina tupu, yeye hakujali akaenda mbali na kufungua chama chake akitetea maslahi ya wananchi na kuibua uozo wa serikali.
Huyu Askofu alitokea kuwa mwiba sana katika kipindi cha uchaguzi wa awamu ya pili ya Rais Mrisho Salehe, ambapo maneno yake yaliyoripotiwa kama ni ya uchochezi yalikuwa yakikiyumbisha chama tawala na kumpa wafuasi wengi sana Askofu huyo.
Kitu cha ajabu ni kwamba pamoja na serikali kumfikisha mahakamani alikuwa akishinda kesi zote, kiasi kwamba watu wakaamini kuwa jamaa anaweza kushinda urais.
Lakini ghafla siku moja tu kabla ya yeye kutangaza kugombea na watangaza nia kutoka vyama mbalimbali kurudisha fomu, inasemekana alipata ajali mbaya sana.
Picha ya vyombo vya habari vilionesha jinsi gari yake iliyobondeka na kupinduka juu chini na huo ukawa ndiyo mwisho wake, japo kuwa wengi wa wafuasi wake walidai kuwa Askofu hakufa na ile siyo gari yake aliyotoka nayo siku hiyo ofisini kwake.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.

ITAENDELEA ALHAMISI

Post a Comment
Powered by Blogger.