MWILI WA SAMWEL SITTA KUWASILI LEO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta unatarajiwa kuwasili leo ukitokea  Ujerumani ambako alikuwa akitibiwa hadi mauti yalipomfika.

Taarifa zilizotolewa na msemaji wa familia ya marehemu, Gerald Mongella, zinasema  mwili huo utawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 9.00 mchana na kupelekwa nyumbani kwake Msasani, Dar es Salaam.

“Ijumaa(kesho) saa tatu asubuhi ibada ya kuuaga mwili huo itafanyika katika viwanja vya Karimjee ambako ndugu na wakazi wa   Dar es Salaam watapata fursa ya kuaga,” alisema Mongella.

Mwili wa Sitta utasafirishwa hadi Dodoma ambako utaagwa na wabunge na baadaye utasafirishwa kwenda Urambo kwa mazishi   Jumamosi.

Sitta alifariki Novemba 07 mwaka huu katika Hospitali ya Technal University alipokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya saratani ya tezi dume.
Post a Comment
Powered by Blogger.