KIWANDA CHA DANGOTE CHASITISHA UZALISHAJI WA SARUJI KUTOKANA NA GHARAMA KUWA JUU

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kiwanda cha Saruji cha Dangote huko Mtwara kimesitisha uzalishaji kutokana na gharama kuelemewa na gharama za uendeshaji hivyo kuwaacha watumiaji wake njia panda.

Hayo yalisemwa na mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Harpeet Duggal Walisema wapo na mazungumzo na serikali kuona namna ya kutatua changamoto hiyo

Mwezi uliopita mkurugenzi huyo alilalamika uamuzi wa serikali kupiga marufuku kiwanda chake kuingiza makaa ya mawe kutoka Afrika Kusini na kutakiwa kutumia ya Liganga ambayo alidai yapo chini ya kiwango na bei ghali.

Pia alilalamikia shirika la maendeleo ya petroli TPDC kwa kushindwa kuwauzia gesi kwa bei rahisi wakati inazalishwa mkoani Mtwara

Waziri Sospeter Muhongo alidai madai yao ya gharama kuwa juu ni ya uzushi.

Chanzo: Nipashe
Post a Comment
Powered by Blogger.