MATANGAZO....
pamoja blogBABA

HABARI

MATUKIO

Michezo imedhaminiwa na

MICHEZO

Simulizi zimedhaminiwa na

SIMULIZI

JAMII

BURUDANI

UCHUMI

MAGAZETI

VIDEO ZETU

» » » » DC CHUNYA AAGIZA TOZO ZOTE ZA VIJIJI NA MALISASILI KUINGIZWA KATIKA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI


Pamoja Blog 11/10/2016 08:11:00 PM 0

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa

Na Mwandishi wetu,Chunya
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa ameitaka halmashauri ya wilaya ya Chunya kuhakikisha kwamba tozo zote za vijiji za Maliasili zinatozwa na zinaonekana kwenye taarifa ya mapato na matumizi.

Aidha ameitaka halmashauri kuingiza takwimu halisi za mazao yote yanayo toka katika maeneo ya vijiji husika.
Agizo hilo, amelitoa leo baada ya kutembelea na kukagua shughuli za kilimo cha umwagiliaji zinazoendelea katika skimu ya Ifumbo, ambayo serikali imewekeza kiasi cha shilingi milioni 900. 

Amesema, licha ya serikali kuwekeza kiasi hicho cha fedha, bado eneo hilo linakabiliwa na changamoto ya ukusanyaji wa mapato kwani asilimia kubwa ya mapato hayo yamekuwa hayakusanywi ipasavyo kutokana na kukithiri kwa njia za panya.

“Serikali inapoteza fedha nyingi na hii inatokana na kutokuwepo kwa mfumo bora wa ufutiliaji wa mazao hivyo mchakato huo utasaidia kuongeza mapato katika Wilaya na halmashauri yenyewe,”amesema.
Hata hivyo, amesema nguvu kubwa iliyopo sasa ni kudhibiti njia zote za panya hasa katika eneo la Shoga ambalo ndio eneo linalotumiwa zaidi na wafanyabiashara wasio waaminifu.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments