RAY C NA DAMIAN SOUL WAINGIA STUDIO KUREKODI PAMOJA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Ukimya wa muda mrefu wa Rehema ‘Ray C’ Chalamila’ uko mbioni kuzimwa kwa kishindo. Ni kwasababu mwanamuziki huyo mkongwe, ameingia studio za Wanene Entertaiment jijini Dar kurekodi kazi mpya.


Muimbaji huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipambana na uraibu wa madawa ya kulevya, amepata mshirika mjuzi wa kumuongoza katika mrejeo wa nguvu – Damian Soul.
“God is good all the time…With my beautiful sister @rayc1982 in the kitchen cooking together with @salthak_tale ..something amazing is coming out,” ameandika Damian kwenye picha aliyoiweka Instagram.


“Happy moment sambamba na my lovely soul sister @rayc1982 in our kitchen @wanenestudios @sarthak_tale …It’s all about love & sharing,” ameongeza kwenye picha nyingine.
Naye Rehema amepost kipande kifupi cha video akiwa na wawili hao na kuandika, “Cooking some delicious food in the studio.”


Picha hizo zinaonesha utofauti alionao sasa Ray C baada ya kupungua kwa kiasi kikubwa huku akiweka matumaini ya kukirejesaha kiuno chake bila mfupa.
Wiki moja iliyopita, alishare pia picha akiwa kwenye studio hizo akirekodi.


Post a Comment
Powered by Blogger.