NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA THEMANINI NA NANE (88)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Usikuusiku, viongozi hao wenye uchu wa madaraka na inda kwa wenzao. Wakaelekea msibani. Kama kawaida ilikuwa ni kwa ajili ya kujionesha tu ili waandishi wa habari wawapige picha na kuonekana kwenye televisheni. 
Walijua lazima wataulizwa maswali kama vile; “unamzungumziaje Marehemu?” naye kama Generali mtarajiwa Hashimu atajibu; “marehemu alikuwa mtu wa watu, mfanyakazi hodari sana, hakika taifa limepata pigo kubwa kumpoteza kiongozi shupavu kama Generali Mwakabuku.”
Hivyo ndivyo kila kiongozi husemaga msibani, kwa hiyo naye akajiandaa kwa hilo.
Wakiwa kwenye magari yao mazito ya kiserikali, wakashuka kwenye nyumba ya Generali Mwakabuku na kuingia ndani ya geti, kila kona kulikuwa kumejaa simanzi tupu.
Waombolezaji wa kiume wakiwa kwenye viti sehemu yote ya ua, wakati wakina mama wakiimba na kulia huko ndani. Viongozi hao wakaingia na kutoa mkono wa pole kwa wafiwa wote waliokuwa katika eneo hilo kisha wakaingia ndani kumfariji mke wa Generali Mwakabuku tena wakionesha wameguswa kweli kwa msiba.
Wakarudi na kusaini katika kitabu cha rambirambi na kwenda kuketi kwenye viti vya wageni wakubwa wakubwa wa serikali.
Lakini hata hapo walishangaa kuonana uso kwa uso na akina Tinonko na wenzake, waliowafuata na kuwapa pole kisha na wao wakaingia ndani kutoa mkono wa pole na kurudi, wakikaa kwenye viti vya kawaida tu.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.

ITAENDELEA JUMAMOSI
Post a Comment
Powered by Blogger.