NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA THEMANINI NA MOJA (81)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Wakati wale viongozi wa jeshi wakitoka nje waliitwa kwenye chumba maalumu, mbele yao akasimama kijana mmoja aliyejitambulisha kwao kwa jina la Eddie ambaye ni mdogo wake Farudume.
Viongozi hao wasingeweza kusubiri na kumsikiliza kijana mdogo kama huyo kama asingekuwa na taarifa muhimu kwao.
“Umesema una taarifa kuhusu Farudume ni zipi?” aliuliza Luteni General, Hashimu Balongo ambaye alikuwa ndiye supervisor wa Farudume ambaye alipotea ghafla ofisini.
“ndiyo mimi ni mdogo wake naitwa Eddie Mamboyoyo. Taarifa ya kwanza ni kwamba, kaka yangu amefariki dunia wiki iliyopita akiwa nyumbani kwake baada ya kuugua kwa muda mrefu.”
“nini?” walishtuka Luteni Generali Hashimu Balongo na Meja General Charles, General Mwakabuku aliyekuwa hajui chochote kuhusu Farudume ikabidi amuulize kwa kumnong’oneza Luteni Generali Hashimu.
“Ni mmoja wa makapteni hapa makao makuu na ndiye aliyejitolea kujenga hilo jengo jipya la Ngome kwa fedha zake mwenyewe,” alisema Luteni Generali Hashimu kwa hisia.
“Pole sana kijana kwa niaba ya jeshi tutahikikisha anazikwa kwa heshima zote, na kulipwa stahiki zake,” alisema General Mwakabuku.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.


ITAENDELEA JUMAMOSI
Post a Comment
Powered by Blogger.