NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA SABINI NA TATU(73)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Baada ya muda yule mlinzi kuondoka walisikia geti likifunguliwa, wao wakajua wameruhusiwa kuingia ndani.
Walifika kwenye jengo kubwa lenye thamani mno na kuelekezwa na mfanyakazi mmoja wapo, aliyewapeleka hadi sebuleni. Pamoja kulikuwa na televisheni kubwa mno ya flat skrini, walishangaa ikiwa imezimwa na mwenyeji wao Farudume akiwa amekaa kwenye kiti huku akiwa amejifunga bandeji kichwani iliyoonesha madonda makubwa.
Kwa mtazamo tu alionekana amepauka sana, huku nyumba ikiandamwa na upweke, kiasi kwamba unaweza ukashangaa mtu tajiri kama huyo anakuwaje hivyo.
“Niwasaidie nini?” alisema Farudume huku akionekana kutoachia tabasamu lolote. Linda na Denis wakaketi na kumtazama Farudume wakiwa tayari kuanza kumuuliza maswali kwa ustadi na weledi tena kwakuwa alikuwa ni kiongozi wa jeshi, walipaswa kujitambulisha wao ni akina nani. ili waweze kueleweka.
Wakati huohuo waligundua kuwa kuna kiharufu fulani kikali kilikuwa kikipita mbele yao na hakikuwa kikitoka sehemu yoyote zaidi ya kutoka kwa Farudume, ambaye baada ya kuwaona wageni wake wakionekana kuboreka na harufu hiyo akatoa pafyumu na kujipulizia kichwani.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.

ITAENDELEA IJUMAA
Post a Comment
Powered by Blogger.