NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA THEMANINI NA TISA(89)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Wakina Tinonko wakiwa pale msibani walikuwa ni jicho na sikio la Generali Mwakabuku aliyekuwa amejificha mbali chini ya uangalizi wa Dokta Aquinas. 
Huko Generali alipiga simu ikulu na kuwasiliana na rais Mrisho ambapo alimueleza mpango mzima wa Luteni Generali Hashimu na Meja Generali Charles. Alifanya hivyo kwa kuwa alijua fika kuwa bila kumwambia, rais atamsimika Luteni Generali Hashimu awe Generali kamili jambo ambalo ni makosa.
Kwahiyo Rais Mrisho alikuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea na ndiyo maana aliacha kwanza kumvisha cheo cha Ugenerali Luteni Generali Hashimu.
Kwahiyo siri hiyo hadi rais alikuwa makini mno kuwajulisha watu wachache wa vyombo vya usalama, hivyo wote hao walikuwa wakichora nyendo za Generali Hashimu na Meja Generali Charles bila wao kujua.
Usiku huo wakiwa wamerudi kutoka msibani, akina Generali Charles walipata taarifa kutoka kwa Seba kuwa tayari wameshamuweka nyoka ndani ya nyumba ya Tinonko na walisikia purukushani ndani, kwa maana hiyo huenda yule mbwa Simba atakuwa ameuawa.
“safi sana, kesho lazima akina Tinonko wataenda pia tena msibani, sasa nataka uandae watu wawavamie hata wakiwa njiani,” alisema Meja Generali Charles na Seba atii amri hiyo.
“Hebu subiri kwanza!” alisema Luteni Generali Hashimu akionekana kama amekumbuka jambo.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.


ITAENDELEA JUMAPILI
Post a Comment
Powered by Blogger.