NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA SABINI NA SABA(77)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“Kitu gani unataka nifanye?” aliuliza Afande Kinyogori kwa hofu.
“utatoka nje na kuelekea moja kwa moja kwenye kambi ya jeshi ya Ngerengere. Wape taarifa waambie ‘kapteni Tinonko storm seals 15,000, BG-15.3” Alisema Tinonko na kumpa Afande Kinyogori kikaratasi cha namba zake za jeshi na za simu na alamaalama nyingine ambazo hakuzitambua.
Kisha akamuongoza Afande Kinyogori hadi nje ya mlango mwingine ulioibukia kwenye mtaro na kutokea barabarani huku akimsisitiza kutothubutu kufungua mdomo wake kuhusu kamera na sehemu alipojificha yeye Tinonko. hiyo ikawa kwa mabadilishano ya kufutwa kwa rekodi ya Afande kinyogori akiua, sambamba na kupewa palepale kitita cha fedha zilizofikia shilingi milioni 10 endapo atafanikisha kutoa taarifa.
Afande Kinyogori kwa muda mchache aliokuwepo ndani aligundua kuwa Tinonko hakuwa mtu wa mchezo, na pia alionekana si wanavyomtaja kama gaidi bali kumbe ni kapteni wa jeshi, alichojua wote waliofika hapo walikuwa wakipiga dili la kutaka kukomba mali zake.
Lakini hata hivyo akajiuliza inawezekanaje, mwanajeshi kama huyo akawa na hela nyingi kiasi hicho, akahisi lazima atakuwa na mchezo mchafu alioufanya.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.


ITAENDELEA JUMANNE
Post a Comment
Powered by Blogger.