NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA SITINI NA SABA(67)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“Kweli nilikuwa namhudumia mama yake, lakini sidhani kama mnachokitaka mtakipata kwa kumshikilia mama mtu ambaye hata uwezo wa kumtambua mtu kwa sasa hana,” aliongea Dr Aquinas lakini Mr Duncan hakuonekana kukata tamaa juu ya zoezi hilo, badala yake alimuamuru Dr Aquinas ampeleke alipo mama huyo haraka iwezekanavyo.
Akilini mwake akaona hawezi kumsaliti rafiki yake, aliona bora afe yeye kuliko kudhurumu furaha ambayo muda mrefu Tinonko alikuwa akiikosa, akabuni mpango wa uongo yaani kuwapeleka wale mabaradhuli sehemu ambayo haikuwa yenyewe.
“Sawa nitawapeleka lakini naomba mnihakikishie kuwa hamtaniua pindi nikiwaonesha mtu wenu,” alisema Dr Aquinas, akiwa na kiraruraru akihisi ikitokea akaharibu tu mpango huyo anaweza kuwa katika hatari ya kifo. Hata hivyo akajipa moyo kuwa bora kufa kuliko kumsaliti rafiki mwema kama Tinonko.
Haraka wazungu wawili, wakaambatana na Dr Aquinas kuelekea kwenye hospitali jeshi ya Lugalo, sehemu ambayo Dr Aquinas alidai kuwa ndipo mama yake Tinonko alikuwa amelazwa na waliamini.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.

ITAENDELEA JUMAMOSI
Post a Comment
Powered by Blogger.