NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA SITINI NA NNE(64)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“Haloo Jackline, toka haraka hapo nyumbani, Peter na Farudume wanakuja,” alisema Tinonko kupitia simu ya kiganja akiongea huku sauti yake ikitetema kwa hofu.
“nini?” alijibu kwa upande wa pili Jackline akionekana amepigwa na butwaa kwa kauli ya Tinonko.
“Hakuna muda ondoka haraka!” alikazia Tinonko lakini wakati simu ipo hewani alisikia kishindo kikubwa kwa upande huo, kisha ukelele wa Jackline. Haraka akajua tayari alikuwa ameshawahiwa na Farudume.
Akakata simu na kuanza kukimbizana na muda akipanda gari lake na kuelekea nyumbani kwa Jackline.
Alipofika alishtukia kuona nyumba nzima ikiwa imegeuka gofu, na alipomtafuta alishangaa kuona hakuna chochote zaidi ya maiti za wakazi wa nyumba hiyo akiwemo baba mwenye nyumba wa Jackline. Hiyo ilimaanisha kuwa tayari Jackline alikuwa ametekwa na Farudume. Wakati huo alikuwa akisikia kelele za mbwa wake na kugundua kuwa muda wote alikuwa amefungiwa ndani ya banda lake ambapo alikuwa akilipigapiga kwa nguvu ili kutoka lakini alionekana kushindwa. Akamfungulia haraka na kuanza kupanga nini cha kufanya.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.


ITAENDELEA JUMATANO
Post a Comment
Powered by Blogger.