NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA TISINI NA MOJA(91)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“Ni amri ya rais Mrisho mwenyewe,” alijibu mtu aliyepigiwa na Meja Generali Charles akafanya hima kukata simu na kumtazama bosi wake uso wake ukiwa umeganda kama barafu.
“Nini!” “Ni rais,” alijibu Meja Generali Charles. Luteni Generali akamtazama mwenzake na kushika kidevu. “Rais anajua au? Na maanisha anajua kuwa wakina Tinonko wana nini?” aliwaka Luteni Generali.
“Inawezekana, maana kama alijua wewe ndiyo umewatia ndani akina Tinonko na amewatoa haraka kiasi hicho basi lazima alifanya hivyo kwa makusudi kabisa,” alichangia Meja Generali. “mbona sina ugomvi na rais? Au labda alipewa taarifa zisizosahihi kuhusu akina Tinonko! Ngoja nimpigie nijue nini kinachoendelea.”
Wakati huo Luteni Generali akampigia rais Mrisho aliyepokea na kuzungumza naye. “habari yako mtukufu rais!”“salama tu, mnaendeleaje na maandalizi ya mazishi?” aliuliza rais.
“Aaha tunaendelea vizuri tu, leo tumepata taarifa kuwa maziko ni kesho kwa hiyo kuaga tutaanzia pale Karimjee. Kila kitu kipo sawa kabisa,” alijibu kwa kujibaraguza Luteni General.
“Mbona umenipigia usiku huu kuna nini unataka kuniambia?”
“Kuna watu kadhaa tuliwakamata na kuwahoji polisi kwa mauaji, lakini tumepata taarifa kuwa umewaruhusu waondoke, kama Luteni Generali naomba kuuliza kwa nini uliwaachia?” “Luteni Generali, watu unaowazungumzia si ni akina Kapteni Tinonko na wenzake, huwajui?”

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.

ITAENDELEA JUMANNE
Post a Comment
Powered by Blogger.