NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA THEMANINI NA TANO (85)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Wakati wakijipanga kumtazama nani aliyeingia, walishangaa kuona kila kitu kikiwa sawa,lakini bado simba alikuwa akipiga kelele. 
Njia pekee ya kujua adui alikuwa wapi ni kumfungulia simba mnyororo wake uliokuwa ukimzuia asiende anapotaka, hivyo wakamuachia akatoka mbio na kuelekea kwenye kona ya ukuta upande wa nyuma ya nyumba.
Akina Tinonko na wenzake wakawa wanafuata kwa nyuma kwa tahadhari. Walipochungulia walishangaa kuona mtu mmoja akishindana na simba aliyemng’ata bara bara kwenye mkono wake aliobeba bastola.
Lakini kwa upande mwingine wa ukuta alionekana mtu mmoja akipenyeza mkono kwenye ukuta ili apande.
Komando Beka kama upepo alinyooka haraka na kufyatua risasi kwenye kiganja cha mkono kilichoshikilia ukuta. Sauti ya maumivu ya mtu ikasikika kwa nje, akipiga makelele. Wakati huo yule mmoja wa ndani akashangaa akiwa amezungukwa kila kona.
Tinonko akatoka nje ya geti na kumdhibiti huyo mmoja waliyemtwanga risasi ya mkono kwa ndani, lakini nje waliona tu michirizi ya damu, iliyoishia kwenye barabara ya lami.
Haraka wakarudi ndani wakiwa na uhakika hakuna hatari nyingine, wakaanza kumhoji mtu huyo ni nani? na kwanini alikuwa hapo. “nyinyi mnadhani mnaweza kunifanya nini mimi?” alisema Rama akijiamini kuliko japo kuwa alikuwa mbele ya majitu matano.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.ITAENDELEA JUMATANO
Post a Comment
Powered by Blogger.