NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA THEMANINI NA MBILI(84)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Usiku ulipoingia Uku-Uku na Linda walijikuta mikononi mwa Rama na Seba, waliofungashwa kama mizigo wakisubiri hatma yao.
“Bosi tumemkamata Uku-Uku lakini alikuwa na Linda yule mlimbwende,” alisema Seba, agizo likatoka kuwa wamfyekelee mbali Linda na kumpeleka Uku-Uku mikononi mwao.
Uku-Uku akajikuta akishuhudia mpenzi wake akiuawa kwa risasi mbele yake kisha yeye akabebwa kwenye gunia na kupelekwa hadi mikononi mwa Luteni Generali Hashimu na Meja Generali Charles waliofanya lile jengo alilokuwa akilitumia Farudume kuwa kama makazi kufanyia unyambisi wao.
“kwa hiyo wewe ni mbirikimo, mwenye uwezo mkubwa mno!” alizungumza Luteni Generali Hashimu akimuuliza Uku-Uku ambaye bado alikuwa na machungu mno ya kuuawa kinyama msichana pekee aliyempenda na kumfanya awe binadamu wa kawaida. Hivyo akafunga mdomo wake na hakujibu chochote.
“Bora uanze kuzungumza siri zenu zote sasa hivi, kabla hatujatumia nguvu kwenye hako kamwili kako kadogo,” alipiga mkwara Meja Generali Charles. Bado Uku-Uku hakujibu kitu.
“Rama, Seba, endeleeni naye akiongea mtupe taarifa,” walisema mabosi hao wa jeshi na kuondoka zao,


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.


ITAENDELEA JUMANNE
Post a Comment
Powered by Blogger.