NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA SABINI NA TANO(75)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Tinonko kwa upande wa pili akiwa na simba, alitazama kila kitu kilichotokea kupitia mitambo ya CCTV. 
Tukirudi nyuma ni kwamba, kabla ya hao maharamia hawajafika kuvamia nyumbani kwa Tinonko, mwenyewe Tinonko aliona njia pekee ya kujitetea si kupambana tu moja kwa moja, badala yake ni kupambana kwa kutumia akili yote.
Hapo akaona njia pekee ni kutumia udhaifu wa vyombo vya dola; fedha. Akaandaa subule kwa kumwaga fedha kibao, alijua fika kuwa ikiwa atatumia tekniki fulani za kutisha. Watu hao hawatakuja wote ndani bali wataingia wachache wachache na pindi wachache hao watakapoingia na kuona fedha nyingi kiasi hicho kwenye sebule, basi lazima wataingiwa na tamaa na kusalitiana wenyewe kwa wenyewe.
Lakini pia aliamua kutegesha kamera ili kuchukua ushahidi wa yote ambayo aliyatarajia yatatokea. Kwa kupitia kamera aliyoitega kwenye taa ya sebuleni hapo, aliwashuhudia wale askari watatu wa mwanzoni wakiingia ndani na walipoona kiasi kile cha fedha kila mtu aliingia tamaa. Mmoja wao akawageukia wenzake na kuwapiga risasi.
Baadaye akapiga risasi nyingine kwenye kochi nadhani alitaka isikike hivyo ili ijulikane kuwa wote watatu wameshambuliwa. Kwa milio hiyo mitatu ndiyo ikatoa ujumbe nje kuwa huenda askari hao wote watatu walipigwa risasi na Tinonko, kumbe wala yeye alikuwa ametulia akiwachora jinsi watu wanavyouana kisa tamaa ya fedha isio yao.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO ILIYOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 UTATUMIWA.

ITAENDELEA JUMAPILI
Post a Comment
Powered by Blogger.