MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP ERNEST MANGU AONGOZA MATEMBEZI YA PAMOJA YA MAOFISA NA ASKARI WA VYEO MBALIMBALI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


     Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu (wapili kushoto) akiwaongoza maofisa na askari wa vyeo mbalimbali wa jeshi la Polisi wakati wa matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya na kujenga ushirikiano mahala pakazi katika mkoa wa kipolisi kinondoni mapema leo asubuhi. Kushoto kwake  ni kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Suzan Kaganda.
Baada ya mori kupanda mchakamchaka ukaanza
 Mchakamchaka na nyimbo za hamasa
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu, akiwaongoza maofisa na askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi katika matembezi ya pamoja ambayo yalianzia katika kituo kikuu cha Polisi Oysterbay na kupita maeneo ya kwa Msasani kwa Mwalimu Nyerere na baadae kuingia barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi.

 Askari Polisi wa Kikosi cha kutuliza ghasia FFU wakiwa katika matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya na kujenga ushirikiano mahala pakazi katika mkoa wa kipolisi kinondoni, matembezi ambayo yaliongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu, mapema leo asubuhi.
   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu (watatu kulia) akiwaongoza maofisa na askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi kufanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya na kujenga ushirikiano mahala pakazi katika mkoa wa kipolisi wa Kindondoni mapema leo asubuhi. (Picha zote na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi)
Post a Comment
Powered by Blogger.