MFALME WA MOROCCO KUJENGA UWANJA WA MPIRA DODOMA, UTAKUWA MKUBWA KULIKO WA TAIFA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amemuomba Mfalme wa Morroco, Mohammed VI kujenga uwanja wa mpira wa miguu mkoani Dodoma.

Akiongea kwenye mkutano wake na Mfalme huyo Ikulu jijini Dar es Salaam, Jumatatu hii wakati wakisaini mikataba 21 na nchi hiyo, Rais Magufuli amesema kuwa amemuomba mfalme huyo kujenga uwanja huo ambao utakuwa mkubwa zaidi ya Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.
“Nimemuomba Mfalme ajenge msikiti mkubwa hapa jijini Dar es Salaam. Lakini pia nimemuomba atujengee uwanja mkubwa wa mpira Dodoma ambao utagharimu kiasi cha dola milioni 100 ambao utakuwa mkubwa zaidi ya huu wa taifa, vyote amekubali atajenga,” amesema Rais Magufuli.
Uwanja huo utatarajiwa kuchukua mashabiki zaidi ya elfu sitini ambao ndiyo idadi ya mashabiki inayochukuwa kwa sasa uwanja wa taifa wa jijini Dar es Salaam. Mfalme huyo yupo nchini kwa ziara ya siku tano.
Post a Comment
Powered by Blogger.