KIM KARDASHIAN AVAMIWA NA MAJAMBAZI MJINI PARIS

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kim Kardashian anadaiwa kuvamiwa na watu wanaohisiwa kuwa ni majambazi waliokuwa na silaha huku wakiwa wamevaa sare za polisi na sura zao wakiwa wamezificha wakati akiwa hotelini huko mjini Paris alipokwenda wiki iliyopita akiwa na mama yake, Kris Jenner na dada yake, Kendall Jenner kuhudhuria kwenye tamasha la mitindo la Paris Fashion Week lililofanyika usiku wa jana.
Habari hizo zilionekana kumshtua zaidi mume wake Kanye West ambaye alilazimika kuvunja onesho lake alilotakiwa kutumbuiza kwenye tamasha la Meadows Music and Arts Festival, mjini New York ili kupata nafasi ya kwenda kumuona mama watoto wake.
Safari ya Kim kwenye mji huo imeonekana kuwa na mikosi baada ya Alhamis iliyopita kukutana na mkasa wa njemba moja maarufu, liitwalo Vitalii Sediuk kubusu makalio yake.
Post a Comment
Powered by Blogger.