DANIEL STURRIDGE ATUPIA MBILI LIVERPOOL IKITINGA ROBO FAINALI KOMBE LA EFL

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Daniel Sturridge amefunga mara mbili wakati Liverpool ikiitoa Tottenham kwa magoli 2-1 na kutinga robo fainali ya kombe la EFL, na kuweka rekodi ya kutofungwa katika michezo 10.

      Daniel Sturridge akifunga goli la kwanza la Liverpool


Sturridge ambaye jumamosi aliingia akitokea benchi katika mchezo walioifunga West Brom, jana ilimchukua dakika 10 tu kufunga goli kwa shuti la umbali wa yadi sita.Divock Origi aliyeonyesha kiwango kizuri alimtengenezea nafasi mbili Sturridge ambaye alizipoteza, lakini baadaye wawili hao walishirikiana vizuri na Sturridge kufunga goli la pili.
        Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge akifunga goli la pili
Post a Comment
Powered by Blogger.