BREAKING NEWS: ALIYEWAHI KUWA MEYA WA DAR, DR. DIDAS MASSABURI AFARIKI DUNIA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.ALIYEKUWA Meya wa Jiji la Dar es Salaam Dk. Didas Masaburi amefariki dunia.
Masaburi ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), amefariki leo saa 3:30 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), alipokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa za kifo chake zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii kuanzia saa 4 usiku na baadaye kuthibitishwa na wanafamilia.
Akizungumza na ndugu wa marehemu, Dk. Makongoro Mahanga, alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na yupo kwenye maandalizi ya kuelekea nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya vikao.
“Taarifa za kifo ni za kweli ingawa kwa jioni hii sijakwenda hospitali, ninafanya mawasiliano na familia ila taarifa kamili kuhusu msiba zitakuwa zikitolewa na msemaji wa familia ambaye usiku huu tutamteua na kesho tutaeleza kwa undani,”alisema Dk. Mahanga.


Naye Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge (CCM), alisema kifo cha Masaburi ni pigo kwa chama pamoja na wakazi wa jijini Dar es Salaam.
“Ni kweli kaka Masaburi ametotoka (amefariki) usiku huu wa leo (jana) saa 3:30 na alikuwa Muhimbili kwa siku kama tano pale ICU (wodi ya wagonjwa mahututi) na tunamumbea mwenzetu ambaye ametangulia mbele ya haki,” alisema Mnyonge.
Post a Comment
Powered by Blogger.