WAZIRI MKUU ATOA RATIBA YA SERIKALI KUHAMIA DODOMA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Waziri   Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha bunge mjini Dodoma Septemba 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Leo Septemba 16, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha mkutano wa nne wa Bunge la 11 uliodumu kwa muda wa wiki mbili, amesoma ratiba ya serikali kuhamia Dodoma.
Kufuatia ratiba hiyo iliyogawanyika katika vipengele sita, itaishia Juni 2020 ambapo serikali yote itakuwa imehamia Dodoma. Ratiba hiyo imegawanyika katika vipengele vifuatavyo

1. Septemba 2016 – Februari 2017.

Katika kipindi hiki, Waziri Mkuu, Mawaziri wote, Manaibu Mawaziri pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara, na baadhi ya watumishi wa Idara katika wizara watahamia Dodoma.

2. Machi 2017 – Agosti 2017.

Wizara zitafanya uchanganuzi wa gharama zinazohitajika kuhamisha watumishi wengine kutoka Dar es Salaam ili kuwekwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18.

3. Septemba 2017 – Februari 2018.

Watumishi wa Idara za Wizara na taasisi mbalimbali za serikali watakuwa wakihamia Dodoma.

4. Machi 2018 – Agosti 2018.

Kuhama kwa watumishi mbalimbali wa serikali.

5. Septemba 2018 – Februari 2020.

Kuhama kwa watumishi wa serikali.

6. Machi 2020 – Juni 2020.

Katika kipindi hiki, Ofisi ya Rais na Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitahamia Dodoma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitumia wasaa huu kuwataka wakazi wa Dodoma kujenga nyumba mbalimbali za makazi ili watumishi wa serikali watakapohamia Dodoma, pamoja na watu wengine, wapate maeneo ya kuishi.
Post a Comment
Powered by Blogger.