WANAFUNZI 15 WALIOCHARAZA VIBOKO WALIMU WASIMAMISHWA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


WANAFUNZI 15 wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Usevya wilayani Mlele Mkoa wa Katavi wameamriwa kurejea nyumbani kwa wiki mbili kwa kosa la kuwashambulia kwa kuwacharaza viboko walimu wao wawili akiwemo Makamu Mkuu wa Shule, Makonda Ng’oka ‘Membele’ (34) ambaye ameng’olewa meno matano kwa kipigo hicho.
Aidha, wanafunzi hao wanaodaiwa kuwa vinara wa mkasa huo wametakiwa kulipa faini ya Sh 20,000 kila mmoja wao na wametakiwa kuzilipa mara watakaporejea shuleni.
Taarifa kutoka shuleni hapo zinaeleza kuwa kikao cha Bodi ya Shule hiyo kilichokutana mwishoni mwa wiki, kilitoa adhabu hizo kwa wanafunzi hao ikiwataka wasionekane shuleni hapo kwa kipindi cha wiki mbili.
Ofisa Elimu wa Mkoa wa Katavi, Ernest Hinju amethibitishwa kufukuzwa kwa wanafunzi hao akisema kuwa Bodi ya shule hiyo iliketi Septemba 16, mwaka huu shuleni hapo na kufikia maamuzi hayo huku akisisitiza kuwa maelezo zaidi atatoa baadaye.
Walimu hao wawili wameendelea kusisitiza kuwa kuwa hawako tayari kuendelea kufundisha katika shule hiyo huku wakisisitiza kuwa ni fedheha kwao kucharazwa viboko na wanafunzi wao wenyewe, huku mwalimu Gabriel Kambona akiachwa na ngeu kichwani. Mwalimu Kambona alidai kuwa haridhiki na adhabu waliopewa wanafunzi hao.
Post a Comment
Powered by Blogger.