WABUNGE WATOA POSHO KUSAIDIA MAAFA KAGERA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi) George Simbachawene amesema madaktari bingwa zaidi ya 15 kutoka Mwanza wamepelekwa Kagera kwa ajili ya kuongeza huduma kwenye hospitali.
Kadhalika, wabunge wameunga mkono juhudi za serikali na wameridhia kukatwa posho ya siku moja ili kuchangia kusaidia maafa yao.

Hatua hiyo inafuatia muongozo wa mbunge wa Mlalo CCM, Rashid Shangazi aliyeomba kiti kutoa muongozo ili wabunge watoe fedha hizo kama sehemu ya kuomboleza pamoja na waathirika.
Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wa pande zote bila kuangalia itikadi zao.
Hata hivyo, Mbunge wa Tarime vijijini Chadema John Heche alisema chama chake kilishatoa Sh 100,000 kila mbunge lakini kufuatia hoja hiyo na wao wapo tayari kuchangia posho zao.
Post a Comment
Powered by Blogger.