TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA KESHO YASOGEZWA MBELE, KUONDOKA JUMATANO SEPTEMBA 14, 2016

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusogeza mbele kwa siku moja safari ya treni ya abiria ya Jumanne kwenda bara kutoka Dar es  Salaam. Treni hiyo itaondoka Jumatano  Septemba 14, 2016 saa 9 alasiri.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kusogezwa mbele ni kutokana na kipande cha treni kuitoka Kigoma kuchelewa kufika Tabora. Treni hiyo wakati ikienda Kigoma ilicheleweshwa kufika Kigoma baada ya treni ya mizigo kupata ajali kati ya stesheni za Kazuramimba na Luiche..

Uongozi wa TRL unawaomba radhi abiria na wananchi kwa ujumla kwa usumbufu utakaojitokeza
Atakayesoma taarifa hii amwarifu mwenzake.


Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya 
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
 Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Dar es Salaam,
Septemba 12, 2016

Post a Comment
Powered by Blogger.