TANZANIA URUSI ZABADALISHANA UZOEFU WA KUDHIBITI UHALIFU

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa kwanza kushoto), akizungumza wakati wa kikao cha  kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi  nchini Urusi.Kikao  hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira ( kushoto), akiangalia video inayoonyesha jinsi ya kudhibiti uhalifu wa barabarani kwa kutumia kamera maalum, wakati wa kikao cha  kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi  nchini Urusi.Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
 Mtaalamu wa mifumo ya Komputa , Boris Derygin akitoa maelezo kuhusu  mada inayohusiana na udhibiti wa uhalifu wa mitandao wakati wa kikao  cha  kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kushoto  ni Kamishna Msaidizi wa Polisi, SACP Gabriel Mukungu. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
 Mtaalamu wa mifumo ya Komputa, Boris Derygin ,akionyesha karatasi inayoelekeza jinsi ya kuitambua gari iliyofanya uhalifu wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi , SACP Gabriel Mukungu wa Jeshi la Polisi la Tanzania, akielekezwa na Kapteni Vasily Gerasimov wa Wizara ya Ulinzi nchini Urusi, namna  ya kudhibiti uhalifu katika majengo wakati wa kikao cha  kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya nchi hizo. Kikao hicho  kilifanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Post a Comment
Powered by Blogger.