RC MAKONDA AKANUSHA TAARIFA ZA KUKAMATA WATU WANAKWENDA NYUMBA ZA WAGENI MCHANA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paulo Makonda amekanusha kauli zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amewaamuru polisi kufanya msako kwenye nyumba za wageni wakati wa mchana na kuwakamata wataokutwa muda huo.

Akizungumza na mtandao huu alisema hajawahi kutoa maagizo kama hayo, kinachofanyika ni Umbeya umbeya tu.

"Mimi kama Mwenyekiti wa ulinzi na usalama siwezi kutoa maagizo kama haya, kuna watu wanafanya kazi viwandani wengine usiku hivyo wanahitaji kupumzika mchana huwezi kuwazuia,
kinachofanyika ni Umbeya, siwezi kujibu hoja za kimbeya ni ujinga". Alisema Makonda.
Post a Comment
Powered by Blogger.