NWANKWO KANU AIFUNGIA ARSENAL MAGOLI 3 KATIKA MCHEZO WA WAKONGWE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mchezaji Mnaigeria Nwankwo Kanu akitokea benchi ameifungia timu ya wachezaji wazamani wa wakongwe wa Arsenal magoli 3, katika ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya wenzao wa AC Milan.

Hata hivyo Kanu ambaye alidhani kuwa amepangwa katika kikosi kinachoanza alijikuta akilazimika kutoka uwanjani baada ya kuingia kuanza kimakosa, huku Gilberto Silva akimpa tafu kutoka uwanjani.

Baada ya kuingia akitokea benchi Kanu alionekana kutulia mno licha ya kuwa na umri wa miaka 40, alifunga goli la kwanza kwa kichwa, na kisha kuongeza la pili kwa kichwa na goli la tatu alifunga kwa mkwaju wa penati.
Gilberto Silva akimpa tafu Kanu kutoka nje ya uwanja baada ya kungundua hajapangwa kuanza kucheza mwanzo wa mchezo
Post a Comment
Powered by Blogger.