NGASSA AJIUNGA NA KLABU YA FANJA YA OMAN

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Wiki tatu baada kuomba kuvunja mkataba na klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini, Mrisho Ngasa ameungana na mtanzania mwingine Danny Lyanga baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Fanja ya Oman.

Tangu Ngasa aliporejea nchini, alikuwa kimya na hakutaka kuzungumza ni wapi ataelekea baada ya kuvunja mkataba wake na Free State.

Fanja inaongoza ligi ya Oman (Oman Professional League) ikiwa na pointi tatu kileleni baada ya kucheza mchezo mmoja wa ligi ambayo ilianza Jumamosi September 17. Fanja ilipata ushindi wa 3-1 ugenini dhidi ya Jalaan.

Klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1970, inaongoza ligi kwa tofauti ya magoli lakini inalingana pointi na vilabu vya Al Oruba, Al-Khabourah, Dhofar na Oman Club, timu zote zikiwa na ponti 3 baada ya kucheza mchezo mmoja.
Post a Comment
Powered by Blogger.