NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA THELASINI NA SITA(36)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Akatembea taratibu akiukata msitu mnene wa Congo akielekea sehemu aliyoamini alikuwa ni uelekeo wa sehemu ya makazi ya mbirikimo rafiki zake.
Akapiga hesabu kama atatembea kwa mwendo huo hataweza kufika sehemu anayoitaka kwa kutumia wiki na hiyo itakuwa imemfanya afe kabla hajafika sehemu anayotaka kwa kuwa anaweza kuishi kwa siku saba tu kabla yale magonjwa aliyoingizwa mwilini kummaliza.
Kwa kujikongoja akatembea hadi eneo moja la kijito kidogo, akakaa huku akisikilizia maumivu ya miguu na mgongo pamoja na uchovu wa mwili, akafungua begi lake na kutoa matunda machache akala na kupitiwa na usingizi mzito.
Hakutaka afe kabla hajalipa kisasi chake akakaza moyo na kutembea akiamini hata kama atakufa kwa uchungu alionao basi atarudi tena hata kama akiwa mzimu ili mradi awamalize wabaya wake.
Kichwani alikuwa bado anawaza yule mwanajeshi ni nani lakini hakuwa akimpatia jibu. Akawaza ikiwa mtu huyo ameweza kumpa adhabu nzito kama hiyo basi kwa vyovyote huenda alikuwa amewahi kumkosea kosa kubwa sana.
Kwa harakaharaka akaanza kuvuta kumbukumbu za watu ambao alishawahi kuwafanyia jambo baya la yeye kustahili adhabu nzito kama hiyo, lakini hakuwaona kwa kuwa hakuwa mtu wa roho mbaya ambaye anaweza kumuumiza mtu bila sababu.
Akatembea zake taratibu huku akimkumbuka mkewe ambaye taarifa zinasema kwamba anakaribia kuolewa. Hakuwa na muda wa kuuliza kama mimba yake ilikuwa imetoka au lah lakini kwa kuwa alikumbuka alishawahi kuhakikishiwa na wale mbirikimo kuwa mtoto wake atazaliwa. 
Hilo akaliachilia mbali ingawa alifahamu wazi kuwa ikiwa mtu anayemtesa amemwambia habari za mke wake kuolewa, basi lazima pia huyo mwanaume anayetarajia kumuoa mkewe naye ni muhusika wa unyama anaofanyiwa.


  Wakati huo akiwa anatembea kule, Tanzania kwenye lile jengo la Utafiti Dokta Gama na madaktari wenzazke walikuwa wakimtazama Tinonko kwa kamera maalumu zilizokuwa zikipaa juu yake kwa kutumia vindege vidogo ‘drones’ vilivyoongozwa na setelaiti.
  Projekti nzima ilionekana kufadhiliwa na watu wa nchi za nje ambao walikuwa wakivutiwa na mambo ya ajabu ya msitu wa Kongo hasa upande wa tiba na madini ya thamani yanayosadikika kulindwa na mbirikimo wa Kivu.
  Watu hao bila shaka walipata kusikia habari hizi wakaona kuna utajiri wa kutosha kutikisa dunia na kwa kushirikiana na Farudume waliweza kujua kuwa Tinonko alikuwa na siri nzito za msitu huo hasa baada ya yeye kutua katikati ya kambi kimaajabu, lakini cha pili ni kufika akiwa na madini aina ya Ruby na lulu nyingine ambazo zilionekana wazi kuwa hazipatikani kokote zaidi ya Kongo na kwenye msitu huo pekee.
  Leo ndiyo ikaja kugundulika kuwa siri hizo zote Farudume alikuwa akipewa na Kiumbe wa Kimbirikimo aliyeitwa kwa jina la Uku-Uku ambaye ndiye hasa ana asili ya hukohuko Kivu. 
  Unaweza kukumbuka kuwa hata siku ya kwanza UKu-Uku alipoonekana na Farudume alikuwa anajua mambo mengi sana kufanana kabisa na Mbirikimo wa Kivu. Kwa namna moja au nyingine huyo ndiye aliyemfanya Aka-Baka akatabiri kuwa adui wa Tinonko anaonekana kujua baadhi ya teknolojia zao.
  Lakini ilikuwaje Farudume akakutana na UKu-Uku?
 • Historia inaanzia mjini Kinshasa mwaka 1993 ambapo mapambano yalikuwa yakitokea mara kwa mara mjini humo hasa baada ya wafuasi wa serikali ya rais wa Kongo kwa wakati huo, Mobutu Seseseko kuangushwa.
 • Mapigano hayo yaliingiliwa kati na majeshi ya umoja wa mataifa ambayo kikosi kimoja kilitokea Tanzania, wakati huo kikiongozwa na Kapteni John Saliboko. Ndani ya kikosi hicho ndiyo alikuwamo Sajenti Thomas Mamboyoyo ambaye huyu alifahamika kwa jina la kivita kama Farudume.
  Ndani ya miezi kadhaa wakitumikia misheni yao nchini humo, walipata kusikia habari za kuwepo kwa mbirikimo wa ajabu, achana na hawa wakawaida, lakini hao waliitwa mbirikimo wa Kivu wenye mali nyingi sana.
  Tamaa iliwakuta wanajeshi hao waliokuwa lindoni na kuamua kuingia msituni kusaka mali hizo kutoka kwa mbirikimo hao. Wakiwa wamepitia shuruba za kila aina, hatimaye wanajeshi wote kutoka Tanzania walikufa njiani kwa magonjwa na kushambuliwa na wanyama wakali, wakimuacha Thomas Mamboyoyo peke yake tena akiwa hoi nusu kufa.
  Akiwa hajui kama amekaribia katikati ya makazi ya mbirikimo hao, Thomas Mamboyoyo anadondoka chini kwa njaa na magonjwa, akilini akimfikiria mdogo wake ambaye si mwingine zaidi ya yule Eddy tuliyemuona akiwa tahira na mlemavu.
  Alimfikiria huyu kwa sababu yeye ndiye alikuwa mlezi wake pekee kwa kuwa wao walikuwa mayatima, hivyo kifo chake yeye kitakuwa ni msiba mkubwa kwa mdogo wake ambaye alikuwa ndiyo kwanza kidato cha tano.
  Farudume ambaye ni Thomas Mamboyoyo akiwa anasubiri kifo chake, ghafla akasikia makelele ya watu kutoka nyuma yake, mara kukatokea mbirikimo mmoja ambaye alionekana kama vile anakimbia kitu, alipofika kwa Farudume akamnyanyua kimaajabu na kupotelea naye hewani.
  Mbirikimo huyo si mwingine bali ndiye huyu Uku-Uku.

 • ITAENDELEA JUMANNE
Post a Comment
Powered by Blogger.