NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA HAMSINI NA TATU(53)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Aka- Baka na Tinonko walionekana wakiwa wanaota moto asubuhi na mapema katikati ya uwanja, Aka-Baka akamuuliza Tinonko; “Umeona?”
Tinonko akajibu; “nimeona?”
Aka-Baka akachukua kijiti cha ulindi na kukitumbukiza pale katikati kwenye moto ghafla ukatokea mwale wa moto, ukawa mkubwa na katikati yake ukaonesha taswira ya mtu akiwa anatembea. Mtu huyo si mwingine bali ni Farudume.
Aka-Baka akamuuliza tena; “unamfahamu huyu?” Tinonko akavuta kumbukumbu na kugundua kuwa huyo ni kiongozi mkubwa wa jeshi la Tanzania, ambaye alikuwa na mdogo wake aliyekuwa akitumikia mafunzo pamoja naye.
Akakumbuka kuwa mdogo wake huyo hata hivyo hakufanikiwa kumaliza jeshi baada ya kupata majeraha makubwa yaliyomsababishia ulemavu.Tinonko akaikumbuka vyema siku ile aliyolenga shabaha na risasi kurudi nyuma na kumpiga moja kwa moja Eddy. Akafungua kinywa chake na kusema; “Namjua?”
Aka- Baka akamwambia; “Hasira zake zipo juu yako, sijui kwa nini anakutafuta lakini inaonekana ana kisasi cha muda mrefu na wewe kiasi cha kuja huku kukutafuta ili akuue.”
“yupo hapa?” aliuliza kwa mshangao Tinonko, Aka-Baka akaitikia kwa kichwa.
“Huyu ndiye yule mwanajeshi ambaye siku zote alikuwa haonekani uso wake, huyu ndiye mbaya wako aliyekufanyia kila baya,” alisema Aka-Baka na kumfanya Tinonko ashangae zaidi.
“Majibu yote ya maswali yako anayo yeye hakuna jinsi zaidi ya kukutana naye, ili kujua ukweli,” alisema Aka-Baka.
Wakasimama na kuelekea upande fulani katika ya zile pande nne kuu za dunia, kisha wakiwa katikati ya pori, Aka-Baka akapuliza baragumu, mlio ukasikika kila kona.
Ghafla Farudume akasikia akaufuata ule mlio kwa tahadhari kubwa. Akiwa ametokelezea mbele ya uwanja mdogo katikati ya pori akaonana uso kwa uso na Tinonko, akatazama upande mwingine akamuona Aka-Baka.

Akarudisha macho yake kwa Tinonko na kuchomoa bastola yake, tayari kwa kuanza kumshambulia. Wakati huo Kamera za kituo cha Utafiti zote zilikuwa zikichukua tukio hilo kwa ukubwa.
“Farudume najua unataka kuniua lakini naomba niambie kosa langu ni nini kiasi cha kunifanya nipitie ukatili mkubwa kiasi kile?” alizungumza Tinonko.
“Haujui! Mshenzi mkubwa haujui?” alisema Farudume huku akitoa picha ya mdogo wake Eddy na kumuonesha Tinonko.
Tinonko akajikuta akishusha pumzi maana hakuwahi kufikiri hata siku moja kama tukio lile la bahati mbaya litamfanya Farudume amuwekee chuki kubwa kiasi cha kuisambaratisha familia yake kama alivyofanya.
Farudume akaanza kuropoka kwa hasira kila kitu alichomfanyia Tinonko kuanzia kuharibu familia yake na la mwisho kabisa ni suala la kuhakikisha amemuua mkewe kisha yeye kumuwekea magonjwa na mbaya zaidi akafunguka kuhusu mpango wao wa kufikia hazina inayomilikiwa na mbirikimo.
Wakati anayaongea hayo hakujua kama Tinonko na Aka-Baka tangu zamani walishajua kama Jackline hakufa kwenye mlipuko wa Farudume hivyo akamuacha aendelee na maneno yake.
Sasa ikawa wazi kwa Tinonko kuwa kumbe kila kitu kwenye maisha yake ye jeshi kilikuwa ni uongo mtupu, hata yeye kupanda cheo haraka ilikuwa ni kwa ajili ya kutengenezewa mazingira ya kutumiwa kutajirisha watu na kulipizwa kisasi.
Tinonko alijikuta akikasirika sana na kupata nguvu ya kutaka kupambana ana kwa ana na Farudume.
Haraka Aka-Baka akiwa tayari amefahamu kuwa kumbe aliyekuwa akimsaidia Farudume si mwingine bali ndugu yake Uku-Uku naye akapandisha hasira zake, akaongea maneno ambayo hayakufahamika ghafla vumbi kubwa likatokea akamshika mkono Tinonko na wote wakapotelea hewani.
Farudume akiwa na hasira zilizopitiliza akapiga risasi hewani na kuambulia patupu, saa hiyohiyo chopa zipatazo nne zilitua katika pori hilo na makomando zaidi ya kumi walitua wakielekea sehemu ambayo waliamini wataweza kuipata hazina ya mbirikimo.

Farudume akiwa na mahasira yake aliendelea kumtafuta Tinonko kila sehemu lakini alishindwa kumuona popote. Wakati huo wale makomando walikuwa wakihangaika kila mmoja wao akitafuta sehemu ambayo waliamini hazina hiyo ipo tena hesabu zote zilionesha kuwa ilikuwa karibu kuliko walivyokuwa wakifikiria.
Wakati huohuo Tinonko na Aka-Baka wakiwa wamefahamu ukweli wa mambo yote likiwemo hili la kuwatuma watu wafike katika msitu huo wa Congo kwa ajili yakuchukua mali za Mbirikimo, walitengeneza mpango wakatumia madawa fulani ikawa kiini macho na kijiji chao kikaonekana kama bwawa kubwa la maji.
Basi wale makomando katikati ya msitu huo wakawa wanazunguka palepale siku nzima hadi wakachoka.
Baada ya kuona mpango wao umetimia Aka-Baka, Twa na wale wananchi wa Mbirikimo wengine wakamuaga kwa mara ya pili mpendwa wao. Kama kawaida Aka-Baka akachora michoro pale ardhini kisha kumkabidhi Tinonko kila aina ya zawadi kisha akamwambia; “sasa umefahamu kila kitu hakikisha unarudi kwa mkeo,”
Jackline wakati huo alikuwa akitoka bafuni kuoga akafungua mlango na kutokea chumbani akijiangalia kwenye kioo jinsi tumbo lake lilivyozidi kuwa kubwa. Ghafla akahisi ameona mtu nyuma ya kioo. Akageuka na kukutana uso kwa uso na Tinonko ambaye alikuwa akimtazama akiwa ameketi pale kitandani. Jackline alijikuta akipiga makelele.
Peter aliyekuwa nje akakimbilia ndani haraka kumsaidia bosi wake, alipoingia chumbani hata yeye hakuamini pembeni ya Jackline alikuwa amesimama Tinonko.
“usiogope mke wangu ni mimi,” alisema Tinonko na kumfuata Jackline na kumkumbatia.
Peter akatoa macho akimtazama Tinonko asijue akimbie au abaki.

KUNA WATU WANACOPY HII STORY NA KUUZA KUANZIA KESHO UTARATIBU WA KUSOMA SIMULIZI HII UNABADILIKA WASILIANA NASI KWA NAMBA HII 0713363965 KUITIA WHATSAPP

ITAENDELEA JUMAMOSI
Post a Comment
Powered by Blogger.