NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA AROBAINI NA TISA(49)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Jackline akiwa anatembea kwa kujikongoja na shujaa wake simba alilazimika mara kadhaa kupitia njaa, kiu na uchovu uliotokana na jua kali la mchana na baridi kali la usiku. 
Lakini kitu kimoja alichojifunza siku hiyo pamoja na kuapa kutoamuamini mwanadamu yoyote tena, lakini alijikuta akiwa radhi kumuamini mnyama ambaye ni simba.
Japokuwa alipitia machungu yote hayo ndani ya muda mfupi lakini kitu cha kupendeza alikuwa akishuhudia wanyama mbalimbali kwa macho yake mawili, tena akiwa mita chache tu kutoka walipo.
Aliweza kujionea makundi ya pundamilia, ngiri, viboko, ndege wa kubwa wa kila aina, tembo, vifaru na wengine wengi ukiachilia wale ambao walikuwa wakimfanya asiwe la lepe la usingizi; ambao ni fisi, chui na simba.
“simba ungekuwa mtu ningekuambia tuelekee sehemu yoyote ambapo kuna barabara ya magari hata ya vumbi. Najua tukipita hapo hata watalii wanaweza kutuona na kutusaidia kuliko huku porini,” alijisemea kwa sauti Jackline mara baada ya kunywa maji ya kijito kidogo kilichokatiza mbele yake na kuungana na mto mkubwa wa Luaha Mkuu.
Mara baada ya kusema hivyo kama vile simba alisikia, alikimbia haraka na kwenda moja kwa moja mbele kisha akasimama na kubweka kwa sauti; “woofh!” Jackline akiwa haelewi nini maana yake akakaza mwendo na kumfuata alipo mbwa huyo. Kilichomshangaza ni kwamba kumbe hapo kulikuwa na barabara ya vumbi na alama ya matairi ya gari yalionekana kupita juu yake.
Jackline akashusha pumzi na kujikuta akimshukuru simba kwa kumpetipeti manyoya yake. Hapo wakaamua kufuata njia hiyo moja kwa moja wakijaribu bahati yao kwa gari lolote la watalii litakalopita na kuwaokoa.


Wakati huo ghafla, nyasi zilionekana kucheza nyuma yao, haraka mbwa simba akasimama kikakamavu na kubweka kwa nguvu zote kwa kiumbe hicho ambacho baadaye kiliibuka na kujidhihirisha kuwa ni chui mkubwa aina ya duma.
Mnyama huyo alionekana kutokuwa na shida na simba bali alitaka kumshambulia moja kwa moja Jackline ambaye kwa hofu alipiga makelele na kujitahidi kukimbia.
Wakati huo simba akahakikisha anapambana kufa na kupona kumlinda mke wa bosi wake na kiumbe alichonacho tumboni. 
Kwa njaa na uchovu aliokuwa nao simba alionekana hawezi kufua dafu kwa chui huyo mwenye njaa ambaye alionekana kumshambulia kwa kasi simba na kumjeruhi vya kutosha mara kadhaa kwa kuzamisha meno na kucha zake ndani ya nyama za simba ambaye hata hivyo mnyama huyo jasiri aliendelea kupambana bila kukata tamaa japokuwa alionekana akiwa karibu na kifo.

***
Siyo mbali na hapo, watalii mke na mume kutoka Italia, mr. Guillemo na mkewe Leornada wakiongozwa na msindikizaji, Erick Malasusa walikuwa wakitalii ndani ya mbuga za Mikumi wakiwa ndani ya gari lao la utalii.
Wageni hawa walikuwa ni waandishi wakongwe wa habari ambao walifika nchini hususani kuandika habari za masuala ya wanyama na uzuri wa Tanzania.
Waliweza kushangaa kila walichokiona, kuanzia twiga, pundamilia na swala, wanyama ambao kwao Italia hawakuwepo. Lengo lao kuu lilikuwa ni kujionea wanyama wanaoitwa simba na hamu hiyo ikawafanya siku chache nyuma wafike katika hoteli ya Guruneti iliyopo ndani ya Simba Campsite.
Baada ya siku nzima ya kutalii na kupiga picha za kila aina za wanyama hao, Mr.Guillemo aliyechomoza kichwa chake juu kabisa ya paa la gari alichukua darubini yake na kutazama huku na huko akifaidi utamu wa Tanzania.


Ghafla Mr. Guillemo alionekana kushangaa baada ya kuona taswira ya kiumbe mwenye rangi nyeupe tupu na mwingine mweusi tii wakipambana na mnyama mwingine aliyeonekana kuwa ni chui au simba.
“Leornada inuka utazame,” Mr. Guillemo alimuita mkewe ambaye alivaa miwani yake vizuri na kusimama kisha naye kuchungulia kupitia darubini ya mumewe, naye akashangaa.
“Erick mnyama gani mwenye manyoya meupe anayepatikana ndani ya mbuga hizi?” watalii hao waliopigwa na butwaa walimuuliza Erick ambaye alikuwa ameketi kwenye gari akiwashangaa wageni wake kwa swali walilomuuliza.
“Mbona hapa hakuna mnyama mweupe, labda hamjatazama vizuri. Naomba nione mimi,” alisema Erick na kuangalia yeye, alichokiona kilimshangaza kama wale watalii. Wakakata shauri wasogee karibu hadi pale alipo mnyama huyo aliyeonekana kupambana na chui akisaidiwa na mnyama mwingine.
Erick akawasha gari na kuelekea kule ambapo alionekana mnyama huyo wa ajabu, wakati huo mzee Guillemo na mkewe wakaandaa kamera zao kwa ajili ya kuhakikisha wanamnasa vizuri mnyama huyo.
Walihakikisha wanafika mita kadhaa ili kutowatisha wanyama hao wasikimbie, hapo mzee Guillemo akachomoza tena na kutazama kupitia kamera yake akavuta na kupiga picha. Akapiga tena kisha akaketi na kumtaka Erick asogee karibu zaidi.
Mara wote wakakumbwa na mshangao baada ya kuona kitu ambacho hawakukitegemea. Kumbe hakuwa mnyama bali ni mwanamke ndani ya shela akipambana na chui huku akisaidiwa na mbwa wake. 
Haraka mzee Guillemo akampa mkewe kamera apige picha kisha yeye akapiga risasi juu na kushuka akijaribu kumuokoa mwanamke huyo na mbwa wake walionekana kuwa na hali mbaya zaidi.

ITAENDELEA JUMANNE

Post a Comment
Powered by Blogger.