NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA AROBAINI NA NANE(48)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Tunachokijua mpaka sasa ni kwamba tangu simba arudishwe nyumbani kutoka jeshini na Sajenti Ngowi, kisha baadaye Peter na Jackline kuhamia Morogoro, hatukumuongelea tena.
Hapa ni kwamba, siku ileile ambayo simba alirudishwa, si Peter wala Suzy waliokuwa wakitaka kumuona mbwa huyo tena akiwa hapo nyumbani akitishia kuwajeruhi, hivyo walimshawishi Jackline kumfungulia mbwa huyo atoke ndani ya nyumba hiyo.
Uzuri ulikuwa ni kwamba, mbwa huyo alikuwa kama vile alivutwa na harufu ya Tinonko ambayo ilikuwa ikitokea makao makuu ya jeshi; Ngome. Hivyo ikawa rahisi, mbwa huyo kutoka hapo nyumbani na kuelekea kulekule alipotokea mwanzo, lakini kutokana na mnyama huyo kuwa na akili alijua hatari inayoweza kumkabili akienda moja kwa moja ndani ya lile jengo alilohisi Tinonko yumo ndani kama alivyofanya siku za nyuma, hivyo akawa anazunguka maeneo hayo na kuvizia nyakati za usiku.
Lakini muda si mrefu, akahisi mtu mwingine ambaye anapaswa kumlinda kwa nguvu zake zote ambaye ni Jackline yupo kwenye hatari. Hapo ndipo akarudi nyumbani kwa kasi na kugundua hayupo isipokuwa harufu yake ikisikika kwa mbali huku nyumba nzima ikionekana kuwa imefungwa.
Hapo Simba akaanza kufuata taratibu njia nzima iliyoelekea barabara kuu ya lami, yaani Morogoro Road.
Kilichomfanya aweze kunusa harufu kwa umbali huo si kingine bali ni ujauzito wa Jackline ambapo kisayansi mama mwenye mimba, mwanamke aliye kwenye siku zake au anayenyonyesha huacha aina fulani ya harufu inayoweza kuvutwa na mbwa kwa umbali mrefu hata wa kufikia maili tano.
Mbwa huyo asiyechoka alianza kuifuatilia harufu hiyo na kuziacha harufu nyingine zote, barabara kwa barabara, akavuka mito na vijito, siku na masaa yakakatika na ndani ya wiki takribani mbili za safari alijikuta akitokea katikati ya jiji la Morogoro kisha harufu ikamvuta hadi katikati ya pori la Mikumi.


Akiwa amechoka na suluba za kutembea, kukimbia na kuokoka mara kwa mara kutoka mikononi mwa wanyama wakali wenye maumbo na nguvu za kutisha ambazo hakuwahi kuziona tangu azaliwe katika ulimwengu wake wa kimbwambwa.
Simba aliona matunda ya kazi yake baada ya hisia zake za harufu zikimpeleka moja kwa moja kwenye kizingiti cha mti ambacho alionekana Jackline akiwa amefungwa huku akiwa hajitambui.
Hapo alitumia kila uwezo wake akang’ata kamba zote na kumfungua mikono lakini bado hakuwa na uwezo wa kumbeba na kuondoka naye. Mbali na hayo hatari kubwa ilikuwa kwa kundi la simba wakali wa mbuga hiyo, walioanza kusogea taratibu wakivutwa na harufu ya mwanadamu katikati ya msitu.
Simba alithibitisha kuwa hakuwa mzuri wa kunasa harufu pekee bali aliweza kupigana na kutumia sauti yake vizuri kuwafukuza makundi ya wanyama hao wakali, usiku mzima hadi pale Jackline alipopata nguvu na kujishtukia akiwa chini ya ulinzi wa mbwa huyo.
Sasa ndiyo aliweza kuona kwa nini mbwa huyo alikuwa akipendwa sana na Tinonko. Akiwa anatokwa machozi ya furaha, akajikuta akimkumbatia mbwa huyo ambaye kwa furaha alikuwa akitikisa mkia wake.
Sasa Jackline alikuwa amerudiwa na kumbukumbu zake vizuri, akakumbuka vyema kuwa akiwa ndani ya gari alishtukia Peter akiendesha gari na kuelekea maporini. Baadaye alikumbuka jinsi Suzy alimziba pua na mdomo kwa kutumia kitambaa kilichokuwa kikitoa harufu kali sana iliyomfanya apoteze fahamu.
“Mungu wangu, walinitupa porini ili nife! Kwa nini sikuyaona haya.. ina maana walikuwa wakitaka mali zangu zote ndiyo maana walinishawishi niolewe haraka hivyo..ohhh Mungu wangu niokoe!” alijikuta akilia kwa uchungu Jackline na kujiona mjinga kwa yote aliyoyafanya.


Upande wake, Farudume alitua katika msitu huu kama alivyotua mwenzake Tinonko, tofauti yao mwenzake alikuwa mgonjwa huku yeye akiwa mzima na mwenye nguvu na akili ya kufanya chochote kwa uharaka zaidi.
Akatazama juu na kuona zile kamera za vindege zilizokuwa zikiendeshwa kutokea kule makao makuu ya utafiti zikiwa juu ya kichwa chake, maana yake alionekana vyema na Mr. Duncan, Dr Gama na wale wazungu wengine.
Alijua hawezi kufanya chochote zaidi ya kuendelea mbele maana hatua yoyote mbaya inaweza ikasababisha mdogo wake au yeye mwenyewe kuingia matatizoni hata kufa.
Bado maumivu ya makali yalikuwa yakimuuma shingoni, akakumbuka ni ile GPS aliyopandikizwa shingoni. Hakika hasira zilimpanda kiasi cha mwisho, akaona jambo pekee la kuweza kufanya akiwa huko Congo hata kama hataweza kuzifikia hazina ni kuhakikisha anamuua Tinonko.
Akawaza, hapo angalau kisasi chake kitatimia kwa kumuua Tinonko. Hilo likampa nguvu, akatembea haraka akifuata nyayo na alama zote alizoonekana amepitia Tinonko kabla yake.
Siku nzima alikuwa njiani na kufanya umbali uliokuwepo kati yake na sehemu alipokuwa Tinonko kuzidi kupungua.
Farudume hakutaka kupumzika alitembea usiku na mchana hatimaye akipita karibu na mto Congo. Kwa kuwa alisikia Tinonko alipona baada ya kutumbukia kwenye mto huo naye aliingia, akaoga na tena akanywa maji ya mto huo, mbaya zaidi hakujisikia nafuu wala jambo lolote la kushangaza.
Akakasirika na kupiga kelele akiita; “Tinonkoooooooo!”
Je, Farudume atakutana na Tinonko, usikose kesho..

ITAENDELEA JUMATATU

Post a Comment
Powered by Blogger.