NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA AROBAINI NA SABA(47)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Mlipuko ulikuwa mkubwa kiasi kwamba hoteli nzima ilitikisika na kufanya watalii wakimbie huku na huko kuokoa maisha yao, ndani ya nusu saa magari ya zima moto yalikuwa yameshafika na kuanza kuzima moto hasa kwenye chumba alichomo Suzy na Peter.
Baada ya muda wa kuzima moto huo, kikosi cha zima moto kiliingia ndani na kukutana mwili mmoja wa ukiwa umeharibika vibaya kwa moto huku mwingine ukionekana kuwa na majeraha ya kuungua kwa moto kila upande lakini ukipumua kwa mbali.
“Mtoeni haraka huyu, anaonekana mzima!” aliongea kiongozi wa kikosi hicho cha zima moto, haraka wakambeba kwenye machela maalumu ya nailoni huku wakiwa wamempaka mafuta ya aina fulani ili ngozi yake iliyoungua isinasie kwenye machela yao na kumsababishia madonda.
Walihakikisha wanaubeba ule mwili mwingine ulioonekana kuungua kuliko kawaida na kuondoka nao wote hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na kuendelea na taratibu zingine.
Mwili huo haraka ulithibitika kuwa ni mfu na ulipelekwa moja kwa moja ndani mochwari kwa ajili ya uchunguzi ambapo matokeo ya ‘autopsy’ (uchunguzi wa mtu alikufa kutokana na nini) yalitoka na kugundua alifariki kutokana na kuripukiwa na kitu mfano wa bomu. 
Uchunguzi huo na ripoti za post mortem za baadaye ziligundua kuwa maiti alikuwa msichana mwenye umri wa miaka 25.
Aidha ripoti kamili iliyofuatiwa na polisi wa upelelezi wa kanda maalumu ya Iringa, walikuwa na taarifa za ziada ikiwemo kuwatambua kama wahanga wa moto huo kuwa ni Peter na Suzy na ni wapenzi waliofika katika hoteli ya Udzungwa siku moja iliyopita.

Hapo hawakuwa na cha kufanya zaidi ya kusubiri Mungu atende miujiza yake ili mgonjwa apone na kuweza kuongea kwa midomo yake kuhusu nini kilichotokea maana tayari uvumi wa tukio hilo kuhusishwa na ugaidi ulikuwa limeanza kusambaa kwa kasi.
Na kweli ilionekana hivyo, maana ukitazama vizuri sekta iliyoshambuliwa ilikuwa ni ya utalii na ndiyo inawaleta watalii wengi wa kizungu nchini, kama wasingesema ugaidi wangesemaje!
Siku tatu zilipita na hali ya mgonjwa ambaye tayari walikuwa wamemtambua kama Peter iliendelea kutengemaa taratibu sana, kiasi kwamba makadilio ya yeye kupona na angalau kurudia hali ya kuweza kuhojiwa yatakuwa takribani baada ya miezi miwili.
Kutokana na mlolongo wa kesi hiyo, jeshi la polisi la kanda hiyo maalumu likamuachia kazi hiyo ya upelelezi Afande Sanga, ambaye kama upelelezi wake utazaa matunda na kuonekana tukio zima kuwa la kigaidi, basi atalazimika kuhamisha kesi hiyo kwenda kitengo cha masuala ya kigaidi na kuwa suala la kitaifa badala ya kuwa la kikanda.
Afande Sanga ndani ya muda mfupi akapata taarifa kuwa Peter alitokea Hoteli ya Gurunet, Mikumi akiwa fungate na mkewe Jackline. Lakini pia taarifa kutoka hoteli hiyo zilidai kuwa sikuk ile Peter alikuwa ametoka kupata ajali mbugani na mkewe huyo kuuawa na simba sambamba na tour guide wake, hayo yalitokea siku hiyohiyo kabla ya kufika hapo Udzungwa.
Swali likawa, je, huyo msichana aliyefariki kwa moto anayeitwa Suzy ni nani yake? na kwanini alionekana kuwepo naye tena sehemu nyingine masaa machache tangu kifo cha mkewe?
Afande Sanga akajiuliza maswali mengi lakini majibu yake yalitegemea uhai wa Peter. Mpaka hapo akaona pengine ni kesi ya wivu wa kimapenzi, lakini hata hivyo haikuwa kesi ya kupuuzia.

Usiku mnene ndani ya msitu mkubwa wa Mikumi alionekana mbwa mmoja mkubwa akibweka kwa nguvu na kutawanya makundi ya fisi walioonekana kumzonga mwanamke mmoja ambaye alionekana kuvalia vazi la bi harusi ‘shela’ huku akiwa ametapakaa damu.
Mbwa huyo alionekana kuwazidi fisi hao waliokimbia hovyo juu ya konde la pori la mikumi. Baada ya kufanya hivyo yule mbwa akamfuata yule mwanamke na kutikisa mkia, hiyo ikawa kama ishara kuwa ni salama waendelee kutembea.
Hata yule mwanamke alipoonekana kuchoka kutokana na kutembea na kuhitaji usingizi, mbwa huyo alionekana amesimama karibu yake na kumlinda kutokana na wanyama wengi wa hatari.
Inasemekana kuwa japo kuwa simba ni mfalme wa mwitu; chui anakimbia haraka na mbwa mwitu kuwa mkali wa kuwinda kwa makundi, lakini mbwa huwa na uwezo wa kipekee kutokana na sauti yake ya kuogofya ya kubweka.
Sauti hii ni tofauti na wanyama wote ambapo mbwa akibweka hata kama kuna simba, chui, mbwa mwitu na wanyama wengine wakali na wakubwa zaidi yake, hukimbia kwa hofu wakidhania ni mnyama mkubwa sana kumkabili.
Hiyo imekuwa ndani ya damu za vizazi vya mbwa wote, nadhani ukweli unaweza ukaupima mwenyewe jinsi vile ulijisikia pindi mbwa akakibwekea laivu.
Siku ya pili jua lilikuchwa na ndiyo sura ya bibi harusi aliyeonekana akitembea peke yake porini ilikuja kubainika na kuwa kumbe ni Jackline. Na yule mbwa kuwa ni kumbe ni simba. 
Je, simba amefikaje hapo? Na Je, Jackline ameponaje kule alipofungwa? Yote hayo utayapata kesho usikose uhondo huu. 

ITAENDELEA JUMAPILI

Post a Comment
Powered by Blogger.