NAJUTA KUMSALITI MUME WANGU SEHEMU YA AROBAINI NA SITA(46)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Huku nako, Peter alionekana akiwa na Suzy, safari ya kutoka hotelini na kuelekea mbugani ikianza huku wakiwa na msindikizaji mmoja wa mbuga za wanyama ndani ya gari yao ya wazi ambayo iliwawezesha kuona kila sehemu kama walivyotaka.
Nao wakajifanya watalii kabisa. Wakati huo Suzy akitambulika kwa jina la Madam Jackline tena akiwa na shela kama bibi harusi huku tumboni akijivalisha manguo aonekane ana mimba.
Hapo unaweza sasa kuona jinsi ambavyo mpango wao unaelekea kuchezeka, yaani ilikuwa lazima Suzy ajifanye Jackline ili kupoteza ushahidi wa kifo cha Jackline. 
Suzy na Peter wakiwa wanaangalia mara kwa mara mandhari ya mbuga hiyo kwa kutumia darubini, hasa baada ya kufika eneo walilokuwa wakilitaka nalo si lingine bali ni simba Campsite. Karibu kabisa na pale walipomfunga Jackline.
Kilichotakiwa kwa Peter saa hiyo ni kumuua yule msindikizaji wao na kumpandisha Suzy kwenye gari waliloahidiana kupita hapo baadaye, kisha yeye atarudi hotelini na kujifanya mkewe Jackline na Msindikizaji wao wameshambuliwa na simba.
Basi wakati akiwaza hayo akaivuta darubini yake na kutazama upande ule ambapo kulikuwa na ule mti walipomfunga Jackline. Kwa kile alichotarajia, kweli aliona mti ukiwa mtupu huku kamba zikiwa zinaning’inia pale. Akamtazama Suzy na kumuoneshea alama ya dole yaani kila kitu kama kalambwanda.
Suzy akakenua meno yake na kusubiri ishara ya pili na hii si nyingine bali ni ya gari ambalo walipanga kumchukua yeye.
Ndani ya dakika chache Peter alipotazama kwenye darubini yake akaona vumbi likitimuka kwa mbali. Huku gari ya mbugani yenye bendera ya njano ikionekana kuja kwa kasi mno.
Hapo Peter akacheka na kumtazama yule msindikizaji wao ambaye kwa bahati mbaya naye alikuwa akiitwa Peter kama yeye, akamwambia:

  “Rafiki, simba hapa ni wengi sana eeh?” aliuliza Peter katili.
  “Yah. Ni wengi sana, lakini leo nashangaa kuona kukiwa kimya hivi,” alijibu yule Peter msindikizaji watalii.
  “ohh au wamehama?” alichagiza Suzy.
  “hahhaa Madam hiyo haiwezekani, jana tu nasikia walikuwa wengi sana maeneo yalee (alisema huku akionesha upande ule ambao walimfunga Jackline). Mwenzangu alikuja na watalii wakachukua picha nzuri sana.”
  Kwa maneno hayo Suzy na Peter wakafurahi kwa pamoja wakajua lazima Jackline atakuwa ameliwa na simba jana kama walivyotarajia. Sasa mpango ukawa mmoja ni kumuua Peter msindikiza watalii.
  Peter akachomoa bastola yake na kumuita Peter yule mwingine nje ya gari, akazuga anamuuliza kitu ghafla bila huruma akamfyatulia risasi ya kichwa iliyotapakaza ubongo wake ardhini. 
  Suzy pamoja na ukatili wake akajificha kwa woga. Wakati huo lile gari lilifika likiwa na dereva ambaye alionekana kufahamiana vilivyo na Peter, Suzy akapanda na kuondoka tayari kumalizia hatua ya mwisho ya mpango wao. 
  Maelekezo hapo yakiwa ni Suzy aondoke na kukutana kesho katika hoteli ya Udzungwa National Park.
  Baada ya Suzy kuondoka, Peter akachukua kipande cha mti na kuking’ata , kisha akachomoa kisu na kujikata kifuani mara tatu; akararua nguo zake.
  Ndani ya dakika chache simba walioonekana kuvutiwa na harufu ya damu ya Peter wawili, walianza kufurika na kuanza kuula mzoga wa Peter. Wakaanza kulizoga na gari alimokuwamo Peter katili.
  Mwenyewe hakuogopa wala nini badala yake akafurahi kuona mpango wake umetimia, akapiga risasi juu. Na kuwatawanya simba wote waliokuwa eneo hilo, kisha akawasha gari na kurudi kwa kasi kule hotelini huku akipiga simu ya upepo ya Peter msindikizaji wa watalii akitoa taarifa ya kumevamiwa na simba.
 • Taarifa za watalii wanandoa kuvamiwa na simba na kuawa porini zilisambaa kwa kasi sana miongoni mwa viongozi pale hotelini. Haraka ‘matour guide’ wasindikiza watalii wa hoteli hiyo ya Guruneti, wakawasha magari yao yaliyosheheni silaha na vifaa vya huduma ya kwanza kuelekea kwenye tukio.
  Wakati huohuo meneja na viongozi wa hoteli hiyo walioonekana kuchanganyikiwa na taarifa hizo haraka wakaitana kwenye kikao maalumu. Ajenda kubwa ikiwa ni kuficha taarifa hizo ili kutowafukuza watalii wao ambao wengi huja kwenye hoteli hiyo kwa sababu ya utalii huo wa wanyama hasa simba.
  Baada ya nusu saa ya kikao hicho wote walitoka hapo wakiwa wamekubaliana kuficha tukio hilo huku wakikubaliana kumfidia mume wa Jackline kwa yote yaliyotokea na kumtaka aondoke haraka hapo hotelini kwao.
  Mpango wa Peter ulionekana kwenda kama alivyopanga huku meneja wa hoteli hiyo akiwa hajui chochote kama huo ulikuwa mchezo aliochezewa na Peter.
  Ndani ya dakika chache tayari Peter alirudishwa hotelini hapo kisiri sana na kupewa matibabu ambayo hata hivyo mwenyewe alinogesha kwa kujifanya kulia na kulalamika kinafki kuhusu kifo cha mkewe Jackline.
  Kama ilivyopangwa siku hiyohiyo tayari alikabidhiwa kitita cha milioni 30 za kitanzania kutoka kwa meneja wa hoteli hiyo. Tena wakiwa wamehgakikisha afya yake ipo sawa. Wakamtaka aondoke siku hiyo hiyo huku wakimpa dokumenti zote zinazohusu taarifa ya kifo cha mkewe kwa akiwa mbugani.
  Chini ya uangalizi wa uongozi wa hoteli, Peter alisindikizwa haraka na kutoka hifadhi hiyo ya Mikumi usikuusiku. Kuanzia hapo mwenyewe akafuatwa na usafiri uleule wa mwanzo uliomfuata Suzy kule porini ambapo alipakia vitu vyake vyote alivyokuwa navyo na kuelekea Udzungwa alipokubaliana na Suzy.
  Suzy alianza kwa kushangaa majeraha ya mpenzi wake Peter lakini baada ya kusikia stori nzima alifurahi sana. Wakati Peter amelala akipumzika. Suzy akakumbuka zawadi ambazo hakuwa amezifungua tangu siku ya harusi.
  Akafungua maboksi kadhaa kisha akayaona mengine mawili akalifuata moja na kulifungua. Ghafla kukatokea mlipuko mkubwa mno.

 • ITAENDELEA JUMAMOSI
Post a Comment
Powered by Blogger.